GODOBLESS LEMA ALITIKISA BUNGE,UFISADI WA LUGUMI CHANZO,SOMA HAPO KUJUA
HOTUBA ya Godbless Lema, Msemaji wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imezuia, anaandika Faki Sosi.
Bunge limeahirishwa mpaka saa
10 jioni baada ya kuzuia kusomwa kwa hotuba hiyo kwa madai kwamba, ina maneno
yanayohitajika kuondolewa ili ikidhi matakwa baada ya kupitiwa na Kamati ya
Kanuni.
Ndani
ya Hotuba ya Lema (Mwanahalisi Online inayo) kipo kipengelea kinachoelezea
sakata la makataba tata wa Kampuni ya Lugumi ambapo Kamati ya Mambo ya Ndani
ilielezwa suala hilo kutojadiliwa bungeni kwa madai tayari lilikuwa limeanza
kuchunguzwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Kipengele
kinachohusu mkataba wa Kampuni ya Lugumu kipo kwenye sehemu ya tano inayoeleza
Mikataba Tata ya Jeshi la Polisi.
Kwa
muda mrefu mkataba huo uliotolewa na Jeshi la Polisi nchini kwa Kampuni ya
Lugumi Enterprises Ltd wenye thamani ya Sh 37 bilioni umedaiwa kuwa na harufu ya
ufisadi.
Mwaka
2011, kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kufunga mashine za alama za vidole katika
vituo vya polisi 108 nchini na kulipwa Sh 34 bilioni kati ya Sh 37 bilioni sawa
na asilimia 99 ya malipo yote.
Mkataba
huo umeonekana kuwa na utata mkubwa na kusababisha sintofahamu kutokana na
kukosekana kwa maelezo yaliyonyooka.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni