DC. BAGAMOYO AKABIDHI MADAWATI 50 KWA SHULE MBILI ZA MSINGI.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed Mwanga,kulia mwenye miwani. akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Majengo madawati. |
Bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid
hemedi Mwanga amekabidhi madawati 50 kwa shule mbili za msingi ikiwa ni mkakati
wa mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everisti Ndikilo wa kuondoa uhaba wa madawati
unaozikabili shule za mkoa wa Pwani.
Madawati hayo 50 yenye thamani ya
shilingi milioni nne yamekabidhiwa kwa shule za msingi Majengo na Mbaruku zote
za Bagamoyo mjini.
Majidi amewashukuru wadau wa
maendeleo ya elimu wilayani Bagamoyo ikiwemo kampuni ya Kirai Pateli ambayo
ndiyo imetoa madawati hayo 50 ili kuondoa tatizo hilo kwa shule za serikali
huku Shubashi Pateli amtoa ahadi ya kutengeneza madawati yote yanayohitajika
kwa shule za Bagamoyo ambayo ni 1,353. Ili kwenda sambamba na agizo la mkuu wa
mkoa wa Pwani ambae amesema mpaka kufikia tarehe 30 may shule zote za mkoa wa
Pwani ziondokane na uhaba wa madawati
Aidha, amewataka wadau mbalimbali wa
maendeleo ya elimu wilayani Bagamoyo kuendelea kuchangia mahitaji mbalimbali ya
elimu katika wilaya ya Bagamoyo na kuongeza kuwa mara baada ya kukamilisha
madawati yanayhitajika kwa shule zote wilaya imepanga kuanza kazi ya umaliziaji
wa maabara za shule hivyo michango inahitajika kutoka kwa wadau mbalimbali ili
kufikia malengo
Kati ya madawati hayo 50 ishirini na
manane yamekabidhiwa kwa shule ya msingi Majengo huku Ishirini na mawili
kukabidhiwa kwa shule ya msingi Mbaruku na kumaliza tatizo la madawati kwa
shule hiyo ya mbaruku.
Awali akiongea mbele ya mkuu wa
wilaya mkuu wa shule ya msingi Majengo Andulile Lukama amesema shule ya Majengo
ina madawati 250 na ina upungufu wa madawati 109 na kwamba inakabiliwa pia na
upungufu wa vyumba vya kusomea hali inayopelekea wanafunzi kuingia kwa zamu
ambapo darasa la nne na la sita wanalazimika kutoka saa saba ili kuwapisha
darasa la tano na la tatu.
Aidha, mwalimu mkuu huyo wa shule ya
msingi Majengo Andulile Lukama na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Anna Kisonso
wamemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa juhudi ya kutafuta wahisani ili kusaidia kuondoa
changamoto zinazozikabili shule za serikali wilayani hapa.
Wakati huohuo Mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo Majid Hemed Mwanga, amewataka walimu wakuu wa shule zote za Bagamoyo
kuacha tabia ya kutumia madawati ya shule kwa shughuli za mikutano ya hadahara.
Majid amesema kuwa madawati ni
kwaajili ya wanafunzi kusomea hivyo ni marufuku kuytatumia kwaajili mikutano
ambayo haihusiani na shule
Amesema kitendo cha kutoa madawati
nje kwaajili ya mikuatano mbalimbali kinachangia uharibifu wa madawati hayo na
baadae kupelekea usumbufu kwa wanafunzi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni