YAMETIMIA YALIOSEMWA NA GAZETI LA MAWIO YATOKEA SASA,SAMSON MWIGAMBA AMWAGA MANYANGA ACT WAZALENDO,SOMA HAOI
SAMSON Mwigamba, Katibu Mkuu wa Chama cha
ACT-Wazalendo ameng’atuka rasmi nafasi hiyo kwa madai kuwa anaenda masomoni, anaandika Pendo Omary.
Anna Mghwira, Mwenyekiti wa
chama hicho amekiambia chanzo changu kuwa, Samson Mwigamba ataanza masomo ya
shahada ya Uzamili ya Biashara (MBA) katika Chuo Kikuu cha Kenyata tawi la
Arusha kuanzia mwezi Mei mwaka huu.
“Kufuatia
hatua hii ameomba aruhusiwe kung’atuka nafasi yake ya Katibu Mkuu wa chama. Katika
kikao chake cha dharura kilichofanyika jana katika Hotel ya Kebby’s Jijini Dar
es Salaam, Kamati ya Uongozi Taifa imeridhia ombi la Katibu Mkuu,” amesema
Mghwira.
Mghwira
amesema kufuatia hatua ya kung’atuka kwa Mwigamba, Kamati ya Uongozi ya chama hicho
imeiagiza kamati ya Mafunzo na Uchaguzi ianze mchakato wa kumpata katibu mkuu
mpya kwa kuzingatia katiba na kanuni za uchaguzi wa chama.
Aidha,
Mwigamba amesema hatua hiyo haimzuii kushiriki katika shughuli zingine za chama
atakapohitajika na akawa na muda wa kutosha.
“Mimi
ni mwanachama mwanzilishi wa ACT- Wazalendo. Nikipata nafasi nitaendelea
kukitumikia chama. Japo nimekuwa kiongozi wa chama katika mazingira magumu.
Kuanzisha chama bila mapato inakulazimu kuchangisha watu na wakati mwingine
vyama kuwekwa mifukoni mwa watu,” amesema Mwigamba.
Haya
yanajiri ikiwa ni miezi takribani mitano tangu gazeti la Mawio lililofutwa na
serikali kuandika juu ya uwezekano wa Mwigamba kuondolewa katika cheo hicho ili
Zitto Kabwe aweze kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu kumwezesha kufanya kazi za
utendaji za siku kwa siku ndani ya chama.
Iliandikwa
kuwa Mkuu huyo wa chama ameandaa na kuratibu mkakati wa kumg’oa kwenye uongozi
Katibu Mkuu, Mwigamba.
Taarifa
zilisema kuwa Zitto anampindua Mwigamba ili achukue wadhifa huo, baada ya
kubaini cheo cha kiongozi mkuu wa chama, hakina nguvu kiutendaji.
Vyanzo
vyetu ndani ya ACT Wazalendo viliarifu kuwa kama mkakati huo ungefanikiwa Zitto
angekuwa katibu mkuu, nafasi yake ya “ukuu wa chama” atapewa Mghwira.
Taarifa
zilizoandikwa na Mawio zilidai kuwa kuwa mkakati huo ulianza katikati ya
Septemba 2015 na ulipaswa kukamilika ndani ya miezi minne.
Waliopewa
jukumu la kusimamia mradi huo wametakiwa kuukamilisha “mapema,” ikiwezekana na
uwe tayari ifikapo Januari 2016.
Zitto
alitajwa kuandaa na kuratibu mkakati huo, baada ya kubaini nafasi yake ndani ya
chama (kiongozi mkuu) ambayo kazi yake ni kueneza sera na kutoa ushauri ndani
ya chama, haina nguvu kama nafasi aliyonayo Mwigamba ya ukatibu mkuu.
Katibu
Mkuu ndiye msimamizi mkuu wa utendaji siku katika chama.
Licha
ya kutowekwa wazi, vyanzo vya taarifa viliarifu kuwa zitto akiwa Katibu Mkuu
ataweza kuhusika moja kwa moja na fedha za ruzuku ambazo chama kingepata kama
kingekuwa na sifa ya kupewa fedha hizo kutoka serikalini kulingana na matokeo
ya uchaguzi mkuu.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni