Zinazobamba

MRITHI WA PAUL MAKONDA KINONDONI AJA NA KASI YAKE,AWAJIA JUU WAKAZI WA KAWE,SOMA HAPO KUJUA

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Salum akizungumza na Mmiliki wa Nyumba ambaye nyumba yake ni miongoni mwa Nyumba zilichini ya Udongo,ambapo Nyumba yake mkazi huyo ipo katika eneo hatarishi
 Pichani  aliyevaa koti ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Salum atia amri kwa watendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wananchi wa Kawe kwa Mkwamani ambao wanaishia katika maeneo hatarishi wawe wamehama ndani ya saa saba,
 Sehemu ya Udongo huo,ambao mda wowote unaweza kushuka kwenye Nyumba za nchini
sehemu ya Nyumba ambazo kati ya 30 ambazo wakazi wake wameamriwa kuhama kabla ya saa mbili usiku wa leo



NA KAROLI VINSENT
MKUU wa Wilaya Kinondoni,Salum Happi amewapa mda wa saa saba, yaani mpaka saa mbili usiku wa leo, nyumba 30 za wakazi wa  Kawe mtaa  wa Ukwamani  wawe wameondoka mara moja katika eneo hilo kutokana na kuishi eneo hatarishi.

Mkuu huyo  wa Wilaya ambaye  ameapishwa juzi Alhamisi  na Rais John Magufuli mara  baada ya kuchukua nafasi hiyo iliachwa wazi na Paul Makonda ambaye sasa ni Mkuu wa mkoa  wa Dar es Salaam,

Wakazi hao ambao wanaishi katika Bonde ambalo  juu ya nyumba hizo  kuna udongo pamoja Nyufa za nyumba ambazo  wakati wowote zinaweza kuanguka na kuleta madhara kwa wananchi hao kwa nyumba zao kufukiwa na udongo huo kutokana mvua zinazoendelea kunyesha.
Happi, ametoa agizo hilo mda huu ,mara baada ya kufanya ziara kwenye maeneo hayo ambapo,amesema yeye kama kiongozi wa Ulinzi wa Usalama katika Wilaya hiyo hatakubali kuona wananchi wake wanakufa  kutokana na mafuriko.
Happi,amewataka watendaji wote wa Halmashauri ya Kinondoni wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya kuhakikisha wakazi hao wanaondoka kabla ya kufika saa mbili usiku,
Huku pia akitoa wazo wa wakazi hao kutafutiwa maeneo ya kuhifadhiwa kwenye eneo la shule  mpaka pale watakapopata eneo zuri la kuishi.
Kwa Upande wao Wakazi hao wa ambao wameamliwa kuhama walimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa,hata wao wanatamani kuondoka maeneo hayo kutokana na kufahamu wanaishi eneo hatarishi ila jambo linawazuia ni hawajui wapi watakwenda kushi kutokana na maisha magumu wananayoishi.
Majibu hayo,yalimfanya mkuu huyo Wilaya kuwasihi watafute hata maeneo yoyote ya kuishi ili kuokoa maisha yao ambayo amedai yapo katika hatari kubwa sana.
 wanawaondoa waka


Hakuna maoni