Zinazobamba

MEYA ILALA AFUATA NYAYO ZA RAIS MAGUFULI

 
Mstahiki Meya wa Ilala Charles Kuyeko
Imeelezwa kuwa kutumbua majipu hakuchagui dini, rangi wala kabila, au itikadi yeyote ile bali kunatokana na usimamizi mbovu wa sheria au kutofuata sheria za nchi katika utumisjhi wa umma.


Hayo yameonekana baada ya Mstahiki Meya wa Ilala Charles Kuyeko kuwatumbua watumishi watatu wa manispaa hiyo kwa kutokana na usimamizi mbovu wa miradi ya barabara za wilaya hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mstahiki Meya Kuyeko amesema wilaya yake imejipanga kusimamia miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo ina wanufaisha wanachi wote hivyo kutokana na kikao kilichofanywa na madiwani mwishoni wa wiki wameadhimia kumsimamisha kazi Mhandisi mkuu Japheri Mwigane na watumishi wengine ambao ni Siajari Mahili na Daniel Kiligiti.
Meya amesema watumishi hao wamekuwa wakilalamikiwa kwa muda mrefu na madiwani wa wilaya hiyo lakini wamekuwa hawayafanyii kazi malalamiko hayo jambo ambalo limemplelekea meya kuchukua hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi kutokana na usmamizi mbovu wa barabara, akiitolea mfano wa barabara ya Moshi Bar.
Katika hatua nyingine Mstahiki Meya Kuyeko ameeleza kuwa Manispaa yake imetenga bilioni 85 kusimamia miradi ya maendeleo tofauti na bajeti za miaka iliyo pita hivyo anaimani kutokana na bajeti hiyo itaweza kutatu suala la miundombinu, huduma za Afya, suala la elimu kwa kuongeza vyumba vya madarasa na madawati ambapo wameishaanza kujenga madarasa kuanzia matano mpaka nane kwa shule zenye upungufu.

Hakuna maoni