MBUNGE KUBENEA SASA AWA MBOGO,NI KUHUSU SAKATA LA UDA,AIBUKA NA NYARAKA NZITO ZINAIUMBUA FAMILIYA YA KIKWETE,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni
Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed
Kubenea akionyesha baadhi ya nyaraka za siri za jiji la Dar es Salaam ambazo
wameanza kuzichambua kwaajili za kutambua mali zilizo chini ya jiji la Dar es
Salaam. katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na
Afisa habari wa Ukawa, Gasto Makwembe.
|
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imewakaanga
wanaotajwa kumiliki Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) bila kufuata
utaratibu, anaandika Pendo Omary.
Hatua hiyo imekuja baada ya
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inayoongozwa Ukawa kuzuia Sh. 5 bilioni,
fedha mali ya Kampuni ya Simon Group Limited.
Mama
Salma Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na Ridhwan Kikwete, mtoto wa
rais huyo na Prof. Juma Kapuya, aliyekuwa Mbunge wa Urambo Magharibi wanatajwa
kuwa miongoni mwa wana hisa kwenye shirika hilo.
Simon
Group Limited ililipa fedha hizo kwa halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya malipo
ya ununuzi wa hisa za UDA.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo
la Ubungo amesema halmashauri haikuuza UDA licha ya Simon Group Limited kudai
kununua.
Kwenye mkutano huo ambao pia uliohudhuriwa
naIsaya Mwita Charles, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Kubenea
amesema, mkutano
uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za wenye mali – Baraza
la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba, ulihudhuriwa na watu wanne
tu.
“Kwanza tunataka mtambue halmashauri haikuuza
UDA kwa kuwa, Simon Group Limited wametumia hati ya UDA – mali ya wananchi
kufanya biashara. Haturudishi fedha hizi mpaka tufanye hesabu, tujue kampuni
hii imepata faida kiasi gani.
“Hata
katika mradi wenyewe wa UDA-TR, kumesheheni utapeli. Unaoitwa mkutano mkuu
maalum wa wana-hisa wa tarehe 10 Juni 2011, uliosimamiwa na Didas Masaburi,
aliyekuwa Meya wa Jiji kuidhinisha pamoja na mengine, uuzaji wa hisa za UDA,
haukuwa halali,” amesema Kubenea.
Kubenea
amesema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon Group uliitishwa bila baraka za
wenye mali – Baraza la Madiwani la Jiji na Msajili wa Hazina na kwamba,
ulihudhuriwa na watu wanne tu
“Watu
hawa ni Dk. Didas Masaburi mwenyewe ambaye alikuwa mwenyekiti; Mkurugenzi wa
Simon Group, Robert Kisena ambaye alikuwa katibu; Mwanasheria wa jiji, Isaac
Nassor Tasinga na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Phillip Mwakyusa,” amesema Kubenea.
Amesema,
kwenye mkutano huo Masaburi alitangaza Kampuni ya Simon kuwa ‘imetimiza
masharti yote ya mkataba wa kupewa hisa, mali na uendeshaji wa UDA.’
Ameeleza
kuwa, mwaka 1983, Msajili wa Hazina alitoa asilimia 51 ya hisa na kuipa
Halmashauri ya Jiji huku Serikali Kuu ikibakiwa na asilimia 49 na kwamba,
shirika hili liliwekwa katika orodha ya mashirika ya kurekebishwa na serikali
mwaka 1997.
“Taarifa
ya serikali ya tarehe 3 Agosti 2011 kwenda Kamati ya Bunge ya Miundombinu
inaeleza mkutano huo ulikuwa batili kwa kuwa, ulikiuka Katiba ya UDA, kifungu
namba 45 kutokana na kutotimia kwa akidi na kukosekana kwa msajili wa hazina,”
amesema Kubenea.
Taarifa
hiyo imeeleza, kikao hicho hakikuwa na mamlaka ya kufanya uamuzi, na kuwa
maazimio yote yaliyofikiwa yalikuwa batili.
“Kwa
taarifa hii pekee, serikali ilipaswa kuiondoa Simon Group kwenye uendeshaji wa
UDA ikiwemo kukodishwa mali zake, hadi hapo uchunguzi wa suala hilo
utakapokamilika. Haikufanya hivyo,” amesema Kubenea.
Kubenea
amesema, kwa taarifa hiyo pekee ilitosha serikali kuchunguza na kuwachukulia
hatua wote waliohusika, hasa kwa kuzingatia kuwa, kabla ya kikao hicho, tayari
Masaburi alishapokea barua ya tarehe 28 Februari 2011 kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu iliyomuagiza kusitisha mara moja mchakato wa kuuza hisa za serikali ambazo
hazijagawiwa.
Akinukuu
barua kutoka kwa Waziri Mkuu yenye Kumbukumbo Na. 185/295/01/27, amesema
Masaburi na wenzake waliendesha mkutano huo wakiwa na kabrasha la Katiba ya UDA
ambayo vipengele vyake vilikuwa vinakataza walichokifanya.
“Kipengele
cha 2.0 cha mkataba kinaeleza mauzo ya hisa 7,880,303 ambazo hazijagawanywa
ambapo kwa majibu wa kipengele cha 2.2, mnunuzi alipaswa kulipa kwa awamu kiasi
cha Sh. 1.1 bilioni,” amesema.
Aidha,
anasema malipo ya kwanza ya Sh. 285. 6 milioni sawa na asilimia 25 ya malipo
yalipaswa kufanywa katika kipindi cha siku zisizozidi 14 tangu mkataba
kufungwa.
Lakini
Simon Group haikulipa kiasi kamili kwa mujibu wa mkataba na hata kiasi ilichotoa
ilikilipa nje ya siku zilizotajwa na mkataba.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni