MBUNGE KUBENEA AENDELEA KUFA NA SHIRIKA LA UDA,SASA ALIPUKA NALO BUNGENI,SOMA HAPO KUJUA
SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo ameanzisha tena
mjadala wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) na Mradi wa Mabasi
yaendayo kasi Dar es Salaam (UDART) bungeni jana, anaandika Happiness Lidwino.
Licha ya mapema jana Lawrance
Mafuru, Msajiri wa Hazina kudai kuwa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
iliiuzia UDA hisa kihalali, Kubenea ameendela kupinga kauli hiyo na kuongeza,
UDA imeuzwa kifisadi na taratibu hazikufuatwa.
Kubenea
amesema, hisa za mradi huo ziliuzwa kinyume cha sheria kutokana na tamaa ya
viongozi wachache waliokuwepo madarakani wakati mradi huo ukiuzwa kwa Kampuni
ya Simon Group Limited.
“Ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na kikao cha Baraza la
Madiwani cha kamati ya uongozi wa Jiji la Dar es Salaam na serikali yenyewe
akiwemo Msajili wa Hazina imejiridhisha kuwa, hisa za UDA ziliuzwa kinyume cha
utaratibu, kwa anayejiita mwekezaji wa Kampuni ya Simon Group Ltd.
“Na
kwamba, rasilimali za UDA zinazohamishika na zisizohamishika zilitawanywa
katika mabenki mbalimbali kwa kuwekwa dhamana. Na mwanahisa mkuu wa hazina
hakuridhishwa na uamuzi wa kuuzwa kwa UDA,” amesema Kubenea.
Anasema,
mkutano mkuu wa wanahisa wa tarehe 10 Juni mwaka 2011 uliosimamiwa na Didas
Massaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam katika kuidhinisha uuzaji wa
UDA usiokuwa halali, serikali inajua.
Pia
amesema, Bunge la Jamhuri ya Muungano linajua na kwamba, anashangazwa na hatua
ya serikali kuendelea na uuzaji huo licha ya kujua ufisadi uliofanyika huko
nyuma.
“Mkutano
huo wa kifisadi uliitishwa na watu wanne haukukidhi akidi na ulisimamiwa na mtu
mmoja Massaburi, Robert Kisena ambaye ni Mkurugenzi wa Simon Group;
Mwanasheria wa Jiji, Isack Nasoro; na Philiphs Mwakisa, Mkurugenzi wa Jiji
kwenye mkutano huo ndipo ikatangazwa kuwa Simon Group imekidhi vigezo vya
kuchukua UDA ambapo si kweli,” amesema Kubenea.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni