Zinazobamba

CITI BENKI NA TAMFI YAJITOSA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI,WAJA NA KITU HIKI,SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Katibu Mkuu wa TAMFI Winnie Terry akizunguma na Waandishi wa Habari leo Jijini hapa,




NA KAROLI VINSENT
Tatizo la ajira ni wimbo unaoimbwa kila siku na watu wa rika na jinsia tofauti  huku watalaam wakishauri ni vyema watu wakaamua kujiajiri kwa kuwa mjasiriamali mdogo na baadae kupiga hatua zaidi za kimaendeleo.

Kwa kuzingatia changamoto hiyo ya ajira taasisi inayo jihusisha na wajasiriamali wadogo wadogo TAMFI kwa kushirikiana na Benki ya Citi nchini wameandaa  Tuzo za wajasiriamali  kwa mwaka 2016 ambapo wajasiriamali wabunifu watafaidika na tuzo hizo pamoja fedha kiasi cha shilingi Milioni 45 kwa ushindi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa TAMFI Winnie Terry amesema mashindano hayo yataanza kuanzia mwezi April mpaka mwezi June  mwaka huu ambapo fursa zitatolea kuendana na idadi ya watu, kanda, jinsia na shughuli za kiuchumi, huku vigezo vya ushindi vitalenga biashara inayokua, faida, ubunifu, na fursa za ajira zitakazo patikana kupitia biashara ya mjasiriamali.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa mpango wa tuzo hizo za wajasiriamali utahakikisha unahusisha na kuwatambua wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa kuzingatia nguvu zao katika kuibua biashara katika jamii zao.
PIchani ni Meneja Uhusiano wa Citi Benki Frank Kallage akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini hapa


Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Citi Benki Frank Kallage amesema kuwa Citi Benki itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo ambapo kwani imewekeza fedha nyingi ili (Milioni 100) kujumuisha wadau muhimu ambao watashawishi muiondombinu sera na kanuni zinazoruhusu ubunifu duniani kote.

Hakuna maoni