BILIONEA LUGUMI AIENYESHA SERIKALI YA MAGUFULI,SASA MAZITO YABAINIKA,WAZIRI WAKE AWAPIGIA MAGOTI WABUNGE WA UKAWA,SOMA HAPO KUJUA
NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA
WAKATI sakata la ufisadi wa mkataba kati ya Kampuni
ya Lugumi Enterprises Ltd na Jeshi la Polisi likiendelea kufukuta, imebainika
Sh milioni 500 zilichotwa bila maelezo yoyote.
Habari za uhakika zilizopatikana mjini hapa jana,
zinasema upotevu huo umebainika baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CGA), kufanya ukaguzi wa taarifa za mapato na matumizi ndani ya Jeshi
la Polisi.
Taarifa hizo ziliwasilishwa juzi na Ofisa Masuhuli
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Inspekta Generali wa Polisi
(D/IGP), Abdulrahman Kaniki.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), vigogo hao walishindwa kutoa
maelezo ya kina kuhusu tofauti hiyo ya fedha, mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.
Chanzo hicho kiliiambia Chanzo change , mjini hapa
jana, kuwa wajumbe wote walitilia shaka mkataba kati ya polisi na Kampuni ya
Lugumi ambao zabuni yake ilitangazwa kwa siku moja na kesho yake ukasainiwa.
YALIYOBAINIKA
Chanzo chetu kinasema katika kikao na vigogo hao,
wajumbe wa PAC walihoji taarifa ya utekelezaji wa mkataba huo na kuonyesha hofu
ya kuwapo ‘wingu la ufisadi’ ambalo linahitaji majibu.
“Zabuni ilitangazwa Septemba 22, mwaka 2011 na
mkataba kusainiwa Septemba 23, mwaka huo huo, ndani ya siku moja mkataba
ukasainiwa jambo ambalo ni hatari.
“Jambo jingine linaloshtua, tangu wakati huo mashine
zote wanasema zipo, lakini hazifanyi kazi na swali ambalo wajumbe wanahoji,
inakuwaje wanatoa zabuni bila kufanya ‘visibility study’ ya kina ili kujua
uwezo wa hii Kampuni ya Lugumi kama ilishawahi kufanya kazi ya aina hii ama la.
“Tumejipanga kwa kila hatua, tumemtaka Makamu
Mwenyekiti wetu Aeshi Hilaly, awasilishe taarifa nzima kwa Spika wa Bunge, Job
Ndugai na mwishowe taarifa hii iwasilishwe mbele ya Bunge ili umma ujue namna
watu wanavyotafuta fedha kinyume cha sheria,” kilisema chanzo chetu.
Mbali na hilo, pia kamati imebaini tofauti ya fedha
zilizopo katika mkataba huo ambapo taarifa ya Jeshi la Polisi inaonyesha
walitoa Sh bilioni 37,163,940,127.7, wakati taarifa ya CAG, inaonyesha
zilizotolewa ni Sh bilioni 37,742,913,007, ikiwa na tofauti ya zaidi ya Sh
milioni 500.
“Katibu Mkuu na wenzake, walipotakiwa kutoa maelezo
ya kina kuhusu zilipo Sh milioni 500 walishindwa, wajumbe wakageuka mbogo na
kutaka suala hilo litolewe maelezo ya kina.
“Licha ya hali hii, PAC tulibaki tukijiuliza, hata
kama kulikuwa na ulazima wa kufunga mashine hizi kwa dharura inakuwaje
hazifanyi kazi? Maana kuna kila dalili ya fedha za umma kuliwa mchana
kweupe,” kilisema chanzo chetu.
Pia kamati hiyo ilibani mkataba ulitolewa kwa
‘single source’ (yaani kampuni moja bila kuishindanisha na nyingine), badala ya
tenda kushindaniwa na kampuni nyingi zaidi.
VIGOGO WAHAHA
Baada ya PAC kuendelea na kazi ya kuchambua taarifa
hiyo, kigogo mmoja ambaye anatajwa kuhusika katika mkataba huo, amekuwa akihaha
kuomba nguvu ya wabunge wa Kambi ya Upinzani, hasa wale wanaotokana na vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ili wamnusuru.
“Ninamshangaa huyo waziri (jina linahifadhiwa),
anahangaika bure, eti anasema watu hawampendi na wanamchukia, amefikia hatua ya
kusema PAC inatumiwa na wauza dawa za kulevya.
“Sisi ni wajumbe ambao kila mmoja anajiweza, hata
siku moja hatuwezi kukaa kutegemea fedha za watu, ila tunafanya kazi kwa
masilahi ya nchi yetu na si vinginevyo. Tumeridhika na posho tunazolipwa na
Bunge, hatuna haja ya kutumika kwa mtu yeyote ila tunasukumwa na uzalendo kwa
Taifa letu,” kilisema chanzo chetu.
Katika kile kinachoonekana ni kama maigizo, baada ya
PAC kutaka mkataba na taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa ufungaji wa
mashine za utambuzi wa alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini,
sakata hilo limekuwa likichukua sura mpya kila kukicha.
Uamuzi huo uliibua hisia miongoni mwa jamii ambapo
katika kipindi cha siku mbili baada ya PAC kutaka ripoti hiyo, Kamati ya Bunge
ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, iliingilia kati ambapo mwenyekiti wake,
Balozi Adadi Rajabu, alikiri kupokea mkataba huo.
UTATA
Kampuni ya Lugumi inadaiwa kupewa tenda na jeshi
hilo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole – ‘Biometric
Access’ katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.
Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14
pekee na tayari kampuni hiyo imelipwa Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia
99 ya fedha zote za mkataba.
Katika sakata hilo, inadaiwa Kampuni ya Lugumi
ilipewa zabuni hiyo ikiwa haina uzoefu wa kazi hiyo.
“Wamepewa mkataba sawa, lakini mbona taarifa
zinaonyesha kuwa kampuni hii haijasajiliwa kama Biometric Access Company na
haijawahi kufanya kazi zozote zinazohusu Biometric Access Control?” alihoji
mmoja wa wataalamu.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni