Zinazobamba

BAJETI YA MAGUFULI YAZIDI ANDAMWA,HAKIELIMU WALIA NA WABUNGE,SOMA HAPO KUJUA



PIchani ni Mkurugenzi wa HakiElimu,John Kalage akizungumza na Waandishi wa habari leo mapema Jijini dar es Salaam


NA KAROLI VINSENT
WAKATI ikiwa imebakia siku nne ili kuanza Bunge la kujadili na kupitisha Bajeti ya serikali ya mwaka 2016-2017,Teyari Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Hakielimu imewataka wabunge kuondoa itikadi zao za vyama na kuungana pamoja ili kuishinika serikali kupunguza   fedha za matumizi ya kawaida katika bajeti ya wizara ya elimu,
 
Ili fedha hizo za matumizi ya kawaida zielekezwa kwenye mipango ya Maendeleo ya elimu.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji-HakiElimu,John Kalage amesema wanawataka Wabunge kuuungana na kuishinikika serikali kuetekeleza mpango wa miaka mitano (2015-2020) unayoitaka bajeti ya kawaida na ya  maendeleo kuwa na uwiano wa asilimia 60 na 40.

Amesema Bajeti iliyopo hakizi hali harisi ya Elimu na  imechangia kurudisha maendeleo ya elimu kutokana bajeti ya elimu kuwa ndogo,

Kalage ametolea mfano Bajeti ya Fedha ya mwaka 2015/2016 bajeti nzima ya elimu ilikuwa Bilioni 3,887.kati ya hivyo Bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu ilikuwa  bilioni 604 tu sawa na  (16%) ya sekta nzima,huku bajeti ya matumizi ya kawaida ikiwa ni bilioni 3,282 sawa  na (84%) ya Bajeti nzima jambo analodai ni vigumu elimu yetu kukuwa kwa kuwa na bajeti hii.

Hata hivyo Kalage ameonesha masikitiko yake katika Bajeti hiyo kwa kusema licha upangaji huo wa fedha inayodaiwa kuwa ni fedha ya maendeleo katika sekta ya elimu huelekezwa katika kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,

“Kwa mfano Bajeti ya 2015/16 bajeti ya maendeleo  ilitengwa bilioni 604,lakini nusu ya fedha hizo  bilioni 306 ilitengwa kwa ajili ya mikipo ya elimu ya juu,hivyo bajeti ya maendeleo ya elimu ilikuwa Bilioni 298,sasa kwa hali hii elimu yetu haitaweza kukuwa “amesema Kalage.


Kalage ametumia nafasi hiyo kuishauri serikali kuondoa fedha za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu katika bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu na badala yake amesema fedha  hizo zipangwe katika matumizi ya kawaida ,kwa madai kuwa itasaidia kutoa picha halisi ya matumizi ya maendeleo katika sekta ya elimu.


Katika hatua nyengine,HakiElimu pia wamewataka Wabunge kuitazama kwa umakini dhana ya elimu bure iliotengwa na Rais John Magufuli kwa kuangalia bajeti husika inayokwenda kutekeleza elimu bure kwa madai kuwa Bajeti iliyopo ni ndogo kabisa na hakikizi maitaji harisi.

Hakuna maoni