ASKOFU AICHOKA SERIKALI YA MAGUFULI,AAMUA KUUNGANA NA UKAWA,SOMA HAPO KUJUA
ASKOFU Mkuu wa Kanaisa la The Word Ministries
Tanzania, Damas Thadei ameungana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) dhidi ya serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao
vya bunge, anaandika Dany Tibason.
Askofu Thadei ameshauri
Serikali ya Rais John Magufuli kuachana na mpango wa kuliingiza taifa gizani
kwa kutojua kinachoendelea bungeni, badala yake iruhusu vipindi hivyo kurushwa
moja kwa moja.
Kauli
ya kusitisha matangazo ya moja kwa moja ilitolewa na Nape Nnauye, Waziri wa
Habari, Utamatuni, Sanaa na Michezo, Januari mwaka huu na kukumbana na upinzani
mkali kutoka kwa wapinzani, taasisi na watu wa kada mbalimbali.
Jumamosi
wiki iliyopita, Freeman Mbowe wakati akisoma hotuba kuhusu makadirio ya mapato
na matumizi ya fedha katika Ofisi Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/17
alisema, hatua hiyo inanyima fursa wananchi kuangalia nini wabunge wanafanya
kwa ajili yao.
“Bunge
ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, na wananchi wana haki ya kujua Bunge lao
linavyofanya kazi ili wawe na uwezo wa kuwawajibisha wawakilishi wao iwapo
hawafanyi kazi inavyostahili.
“Katika
hali isiyo ya kawaida, serikali na uongozi wa Bunge, imewapoka wananchi haki
yao ya kupata habari za Bunge kwa kuzuia mijadala Bungeni kurushwa moja kwa
moja na televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya habari vya kujitegemea,”
amesema Mbowe.
Abdul
Kambaya, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Umma wa Chama cha Wananchi (CUF),
alikosoa mpango huo na kudai, serikali inajihami kwa wananchi kutokana na madudu
ndani ya utawala wa CCM.
Askofu
Thadei amesema, serikali inapaswa kuacha kufanya kazi kwa woga na badala yake
ijiamini na kutoa haki kwa Watanzania wanazostahili kuzipata na si vinginevyo.
Amesema,
kitendo cha serikali kutoonesha matangazo ya moja kwa moja ya bunge ni dalili
ya uoga na kuzuia wananchi kuona madudu yanayofanywa na baadhi ya watumishi wa
serikali.
“Kitendo
cha serikali kuficha yanayoendelea bungeni ni kuminya uhuru wa wananchi kupata
habari jambo ambalo ni viashiria vya kuvunja Katiba ya nchi,” amesema.
Amesema,
hata kama serikali itaficha ukweli, upo uwezekano mkubwa kwa wananchi kujua
nini kinaendelea.
Amesema,
watumishi wa Mungu na watumishi wa serikali kazi yao ni moja ambapo ni
kuhakikisha Watanzania wanapata haki zao.
“Viongozi
wa serikali wanahakikisha wanakusanya mapato kwa ajili ya kuwapatia watu wake
maendeleo, wananchi kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanaisimamia serikali.
“Viongozi
wa Dini kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanatunza roho za waumini wao ili
kuondokana na tabia mbaya ambazo zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
“Hivyo
kwa kutambua kwamba, kila mmoja anawajibu wake. Ni vyema mambo hayo yakatimizwa
ili asiwepo mtu yeyote wa kulalamiwa,” ameeleza Askofu Thadei.
Hata
hivyo amesema, staili ya Rais John Magufuli kutumbua majipu inapaswa kufuatwa
sheria na kanuni za utumishi wa umma.
Amesema,
“haya yote ya wizi, ufisadi na ubinafsi unatokana na watu kutokuwa na hofu ya
Mungu, kama watu watakuwa na hofu ya Mungu mambo yote ambayo yanalisumbua taifa
yatakwisha.”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni