ZANZIBAR NI AIBU TUPU,SOMA HAPO KUJUA
Hali ilivyo sasa Zanzibar |
KWA hakika mambo yanayofanywa na Jeshi la Polisi
visiwani Zanzibar ni aibu tupu. Maisha ya Wazanzibari yamepoteza mwelekeo
sababu kuu ni mkakati wa jeshi hilo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kushika nchi, anaandika Hapyness Lidwino.
Maisha ya wasiwasi yanashika
kasi, wananchi wanaishi kwa hofu huku, wanateswa na wengine wanakamatwa na
kuswekwa ndani kwa kuwa wanaonesha kutoridhika na harakati za jeshi hilo na
CCM.
Hata
wale ambao si wafuasi wa vyama vya siasa visiwani humo wanakiona cha mtemakuni,
nchi inaendeshwa kimabavu. Wenye hofu zaidi wanatoroka Pemba.
“Yanayofanyika
hapa yanaweza kukutoa machozi, unyama wanaofanyiwa raia hauna kipimo,
yaliyoelezwa na CUF kuhusu kipigo ni kweli,” anazungumza raia mmoja wa Zanzibar
ambaye ameomba kuhifadhiwa jina lake na kuongeza;
“Yanayofanyika
Zanzibar yanafichwa na yanapaswa kufichwa na watawala kwa kuwa ni aibu, ni aibu
wallah. Kila mpenda amani hawezi kuvumilia, ni lazima atoe machozi yake, hatuna
raha hatuna amani.”
Zanzibar
imeingia kwenye utata zaidi baada ya Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta kinyume cha sheria matokeo ya Uchaguzi Mkuu
visiwani humo tarehe 28 Oktoba mwaka jana.
Yanayotokea
visiwani Zanzibar kwa sasa yalionywa na wasomi, wanaharakati, viongozi wa dini,
mataifa ya nje na wanahabari.
Kumbukumbu
ya Gazeti la MAWIO lililofutwa na serikali tarehe 15 Januari mwaka huu
liliandika kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Z’bar’ ambapo ndio sababu ya
kufutwa kwake. Yanayotokea sasa yanaakisi kilichoandikwa na MAWIO.
Uchaguzi
huo uliopangwa kufanyika kesho umeharibu mwelekeo wa maisha ya Wazanzibar kwa
ujumla, wanaoumia ni wafuasi wa vyama na wasio wafuasi.
Kauli
tata zimekuwa zikipazwa visiwani Zanzibar ikiwa ni kilele cha kuonesha kuwepo
kwa wasiwasi, matukio mbalimbali yameakisi kuwa Zanzibar si salama.
Miongoni
mwayo ni ile kauli ya wananchi wa Pemba kutakiwa kulala kabla ya saa tatu
usiku. Kauli hiyo pia inawahusu wageni (watalii) ambao wametakiwa kurejea
katika nyumba za wageni walimofikia kabla ya muda huo. Hakuna amani Zanzibar.
Jeshi
la Polisi limekuwa likikamata wanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF), wanavamia
ofisi za chama hicho na kuharibu mali zao huku wakiwa na mitutu ya bunduki na
vifaru vya vita. Usalama upo wapi?
Tayari
wafuasi na viongozi wa CUF zaidi ya 60 wamekamatwa na polisi, miongoni mwao ni
Eddy Liamy mwanamikakati ya ushindi CUF; Nassoro Mazrui, Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar; Mahomoud Mahinda, Katibu Mtendaji JUVICUF; Abeid Hamis Bakari, Mkuu
wa Idara ya Habari na Uenezi na Hamad Masoud, Mkurugenzi wa Habari CUF.
Mansoor
Yusuph Himid, Mshauri Mkuu wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif amekamatwa
kwa madai ya kuwa na taarifa za watu waliolipua maskani ya CCM iliyopo Kisongwe
Michenzani Mjini Unguja.
Viongozi
wa CCM wanaotoa kauli tata za kushawishi vurugu wanalindwa, ni Sadifa Juma
Khamis, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVICCM) ambaye amawetaka vijana
wa chama hicho kuwa tayari kwa mapambano.
Ofisi
za CUF, CCM zachomwa moto, wanaokamatwa ni wanachama na wapenzi wa CUF pekee.
Haki ipo wapi? Amani ipo wapi Zanzibar? Mataifa ya kimataifa yapo kimya.
Idadi
ya wanajeshi imeongeza, hofu inatokana na nini? Nani anasakwa? Je hawana kazi
nyingine? Kwanini Serikali ya CCM inatumia nguvu kutwaa mamlaka? Mazombi
wanafumbiwa macho, raia wanakamatwa. Hii nini?
Shangaa
hapa, Hamdan Omar Makame, Kamishna wa Polisi Zanzibar ananukuliwa ‘’sisi
hatujawahi kuwaona hao masombi bali tunasikia tu katika vyombo vya habari.’
Hawa wanaokanwa wanatumia usafiri wa serikali. Zanzibar ni aibu.
Habari hii kwanisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni