Zinazobamba

UWAMADA WAMUANGUKIA Dkt KINWANGALLA,SOMA HAPO KUJUA



 

NA KAROLI VINSENT
WAKATI Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ametangaza maduka yote yanayouza dawa za binadamu  yawe yamefungwa kwa madai kuwa yana wauzaji wasiokuwa na sifa.

Nao Wamiliki wa maduka ya madawa muhimu za Binadamu (UWADAMUDA) wamemtaka Dkt Kingwangara kuangalia njia nyengine na sio kuyafungwa maduka hayo

Akizungumza na Waandishi wa habari  leo Jijini Dar es Salaam,.Mwenyekiti wa (UWADAMUDA),Juma Mganga amesema hoja ya Naibu waziri ya kuyafungia maduka hayo ya lakuwataka wauza madaka hayo yawe na wauzaji wajuuzi ni kuwaonea kwani  amedai sio maduka yote  hayana wauzaji wenye sifa,

“Maduka mengi ya madawa yanawasomia wazuri lakini kitendo cha Naibu Waziri kutangaza yote yafungwe ni kutonea sana kwani sio yote yanatatizo hili,”amesema Mganga,

Mganga amesema kitendo cha maduka hayo kufungwa kumewaathiri sana wauzaji wa dawa kutakana na walikuwa wanapata kipato cha kila siku kutokana na biashara hizo.

“Wauzaji wa maduka haya walikuwa wanatumia kupata kipato cha kuendesha familia,kitendo cha maduka haya kufungwa kimewathiri sana,leo hawapati kipato cha kila siku”ameongeza kusema Mganga,

Mganga ametumia nafasi hiyo kumuomba Rais John Magufuli kuingilia kwani hatua ya kufungwa maduka hayo imewakatisha tamaa kwani hawajui wapi pakwenda.

Hakuna maoni