Zinazobamba

SERIKALI YA MAGUFULI YAENDELEA KUMWANDAMA BILIONEA BAKHRESA,TCRA YAIBUKA NA KUIFUNGIA KAMPUNI YAKE MOJA,PIA ZIPO ZENGINE ZA RUFARO,KAMPUNI ZA SIMU,SOMA



 


NA KAROLI VINSENT
SERIKALI ya awamu ya tano ni kama imekuwa mwiba kwenye kampuni za Mfanyabiashara maarufu nchini, Saed Salim Bakhresa ndivyo naweza kusema  baada ya  kampuni zake hizo   ikiwemo  ya Bandari ya nchi kavu  (ICD ) kuendelea kukabwa koo kutokana na kuikosesha serikali mapato,

Ambapo sasa pia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA)  nayo imerusha rungu kwa ya  Kampuni ya Azam Marine Company Limited  ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara huyo kwa kuitaka kuacha mara moja kuendesha shughuli za kiposta za kusafirisha vifurushi na vipeto baada ya kubainika wanafanya hivyo bila ruhusu ya TCRA  na kuikoseha serikali mapato,

Vilevile,TCRA imepiga Faini ya shilingi milioni 5 kampuni hiyo kutokana na kufanya shughuli hizo,

Sanjari na Kampuni za Bakhresa pia TCRA imepiga faini ya Milioni 10 Kampuni ya Rifaro pamoja na kuizuia kuacha mara moja kutumia rasilimali namba maalumu ya 15420 kutokana na kukiuka sheria za mamlaka hiyo,

Pia TCRA imetoa adhabu kwa kampuni za simu za Airtel Tanzania,Smart,Tigo,Vodacom.Zantel kutokana na kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa TCRA  Dkt Ally Simba ametaja sababu ya kila kampuni kupata adhabu hizo, huku akitabainisha kuwa kampuni hizo zimeshindwa kusimamia sheria za TCRA,

Amesema Kampuni ya Azam Marine Company limited imekiuka sheria ya Mamlaka ya Mawasiliona nchini kifungu cha 172 kama kilivyorekebishwa na kifungu cha 179 cha sheria ya Mawasiliano ya kielekroniki na Posta ,baada ya kubainika walikuwa wanafanya kazi ya usafirishaji mizigo bila ya kuwa na idhini kutoka TCRA kama sheria hiyo inavyotaka,

Amesema TCRA baada kubaini kosa hilo waliwaita watu wa Azam waje kujitetea kwenye Mamlaka hiyo na kusikiliza utetezi wake,ndipo Kampuni ya Azam ilikili kufanya Shuguli hizo bila kibali.

Dkt Simba ameyataja makosa pia kwa Kampuni Rifaro ambapo amesema Kampuni hiyo ilitumia namba maalumu ya (VAS SMS CODE))15420 huku leseni ya kuwaruhusu namba hiyo kuisha mda wake,
 Amesema Kampuni ya Rufaro ilipewa leseni ya Mwaka mmoja yaani 27 Julai 2014 na cheti chake kumalizika 27 Julai 2015 lakini kampuni hiyo iliendelea kutumia namba hiyo mpaka sasa huku akitabainisha kuwa kampuni hiyo imekiuka Kanuni ya  17 ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2011 ambayo inaakataza kufanya hivyo,
“Baada ya kuwaita kujitetea na walipokuja wakakili kutumia namba ambayo mda wake ulikuwa umekwisha basi tumepiga Faini ya milioni 10 kampuni ya Rifaro na kuitaka iache mara moja kutumia rasilimali ya namba maalumu 15420”amesema Dkt Simba.
Hata hivyo Dkt Simba ametaja pia sababu ya kuzitoza Faini kampuni za Simu nchini ambapo amedai kampuni hizo zimeshindwa kutoa hudumu kwa mujibu wa vigezo vya ubora na  huduma kwa mujibu wa kanuni za ubora wa huduma za sheria ya mawasiliano ya kielekroniki na Posta za mwaka 2011,
Dkt Simba amefafanua kwa kusema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha jedwali la pili la sheria ya Mawasiliano ya kilekroniki na Posta sura 306 ambacho kifungu hicho kinaipa nguvu za kisheria Mamlaka kutoa adhabu kampuni hizo kwa kiuka masharti ya Leseni,
Ametaja Kampini hizo ni Airtel Tanzania limited ambayo imepigwa faini ya milioni 25,Kampuni ya Bensoni Informatics Limeted (Smart) nayo imepigwa faini ya milioni 12.5,Kampuni ya MIC Tanzania Limeted (Trading as Tigo)imepigwa faini ya milioni 25,

Zengine ni Kampuni ya Vodacom Tanzania Limeted ambayo imepigwa faini ya Milioni 27.5,na Kampuni ya Zanzibar Telecom Limited(Zantel) nayo imepigwa faini milioni 25

Vilevile Dkt Simba amezitaka Kampuni zote zinazohusika na masuala ya Mawasilioni nchini kufuata taratibu za sheria za TCRA ili kuepuka usumbufu hukua akisema Mamlaka hiyo haitosita kuzichukulia hatua kali za kisheria kampuni zitakazokiuka taratibu za sheria.

Hakuna maoni