MBUNGE KUBENEA UVUMILIVU UMEMSHINDA,AJIANDAA KURUSHA KUMBORA KWA MAGUFULI NA POLISI WAKE,SOMA HAPO KUJUA
Saed Kubenea, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo
SAED Kubenea,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema) amepanga kutoa taarifa itakayowagusa
viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli na Jeshi la
Polisi, anaandika Faki Sosi.
Kwenye taarifa hiyo pia ataeleza taarifa za
kukamatwa kwake zilizothibitishwa na Simon Siro, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar
es Salaam.
Taarifa kwenye vyombo vya habari jana zilieleza kwamba, Kubenea
ni miongoni mwa waliokamatwa na Jeshi la Polisi ambapo Kamanda Siro alidai
kukamatwa kwake.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinaeleza kuwa, anatarajia kutoa
taarifa kwa umma wakati wowote kueleza kile kinachoitwa sakata la polisi,
madiwani na wabunge wa Ukawa wakati wa vurugu za uchaguzi wa meya ulioghairisha
Jumamosi wiki iliyopita.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Ukawa inaeleza
kuwa, Kubenea anatarajia kutoa taarifa ili kutoa ufafanuzi wa ndani kuhusu
tukio hilo.
“Kubenea atatoa taarifa muda wowote kuanzia sasa, kwa kuongea
moja kwa moja na waandishi wa habari, ama kutoa taarifa kwa vyombo vya habari,”
amesema.
Habari hii
kwahisania ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni