Zinazobamba

CCM YAENDELEA KUPORA HALMASHAURI ZA UPINZANI,WATUMIA UMAFIA KUSHINDA HALMASHAURI YA KILOMBERO,SOMA HAPO KUJUA



 Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero akiwa anashikiliwa na polisi katika uchaguzi wa awali
 Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero akiwa anashikiliwa na polisi katika uchaguzi wa awali

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kimekwapua Uenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa ya Kilombero, anaandika Happyness Lidwino.
Uchaguzi huo umefanyika leo Morogoro wilayani humo ambapo David Ligazo wa CCM ametangazwa kushinda kwa kura 19 dhidi ya mpinzani wake G. Lwena wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 18.
Katika halmashauri hiyo, CCM ilikuwa na jumla ya wajumbe 19 ambapo vyama vinavyoundwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiwa 20.
Namna ilivyokuwa
Jeshi la Polisi lilitumika kukamata wajumbe wawili ambao ni wabunge, Peter Lijualikali na Devota Minja hivyo kufanya idadi ya wajumbe wa Ukawa kupungua kutoka 20 na kuwa 18.
Hata hivyo, kwenye uchaguzi huo idadi kubwa ya polisi waliingizwa ndani ya ukumbi ikiwa ni hatua za kuhakikisha CCM inapata ushindi.
Pia baadhi ya waandishi na wananchi walizuiwa kuingia ndani ya ukumbi huo ambapo waandishi walioruhusiwa kuingia ukumbini ni wa Star TV, TBC, Gazeti la Uhuru na Jambo Leo.
Pia, wasimamizi wa uchguzi huo hawakujali kitendo cha polisi kuwazuia wabunge hao kuingia kupiga kura zoezi liliendelea na hatimaye CCM walitangazwa kushinda.

Hakuna maoni