RUNGU LA MAGUFULI LAWAANGUKIA WAPIGA DEBE,SASA WATAKIWA KUKAMATWA MARA MOJA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Waziri nchi
ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane
NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita baada ya Rais John Magufuli
kuwaagiza wakuu wa mikoa wapya kuwakamata vijana wote ambao wanacheza (poolTable) nyakati za asubuhi,kwa madai kuwa wajiingize
kwenye shughuli za ufanyaji kazi,
Naye,Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na
serikali za mtaa,George Simbachawane amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhakikisha anawaaondoa
wapiga “debe” wote kwenye vituo vya mabasi kwa madai kuwa wanafanya vitendo vya
kiharifu.
Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Jijini Dar
es Salaam,wakati wa semina kwa wakuu wa
mikoa wote nchini ambao waliapishwa jana na Rais Magufuli,
Ambapo alitumia nafasi hiyo kwa kusema kazi ya kupiga debe sio rasmi na aina kipato
kitachoweza kumkwamua kijana kuondokana na tatizo la umasikini,
“Yaani hata hapa Dar es salaam namuomba mkuu wa
mkoa ahakikishe anawondoa hawa wapiga
debe kwenye vituo vya mabasi kwani wamekuwa wakichangia kutokea kwa
uharifu,kipato cha mpiga debe kwa siku hakiwezi kumkwamua kimaisha sana sana wanatumia
nafasi hiyo kufanya uharifu wanatakiwa kuondolewa haraka waende kwenye kazi hata za kilimo”amesema Simbachawene.
Hata Hivyo Waziri Simbachane ametumia nafasi hiyo
kuwataka wakuu wa mikoa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwatumikia wananchi
ikiwemo kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni