MKUTANO MKUU WA WADAU WA SUKARI NCHINI WAENDELEA,TAARIFA KAMILI HII HAPO,SOMA HAPO
Pichani ni Mkurugenzi wa World Diabetes Foundation akiongea na
waandishi wa habari kuhusu mkutano wa wadau wa kisukari uliopangwa kuanza
tarehe 17 na 18 katika ukumbi wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere Convention
Centre
MKUTANO huo maalum
wa siku mbili wa wadau wa kisukari duniani ambao utafanyika katika ukumbi wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar Es Salaam, Tanzania.
Mshauri Mganga na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hosipitali ya Shree Hindu Mandal, ambaye pia ni Katibu
wa kitengo cha Watafiti wa ugonjwa wa kisukari Afrika Mashariki (EADSG) Dkt.
Kaushik Ramaiya alisema umuhimu wa mbinu ya Taifa dhidi ya vita ya ugonjwa wa
kisukari ni nyenzo muhimu kwa Taifa hili.
Akiongea na
waandishi wa habari katika uzinduzi wa Mkutano huo Dkt Kaushik alisema
"Linapokuja suala la kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kisukari Mkutano kama
huo unachukua nafasi kubwa kwa wagonjwa waishio na Kisukari,”
"Kwa
kuimarisha kile ambacho tumejifunza, na kubadilishana mambo muhimu miongoni mwa
nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, tutakuwa na uwezo wa
kuwezesha yatokanayo baada ya Kongamano la Kisayansi na utafiti katika kufikia
malengo, Mpango wa WHO Global Action kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza,
unahitajika."
Mkurugenzi Mtendaji
wa Mfuko wa Kisukari Duniani (Wolrd Diabetes Foundation) Dkt Anders Dejgaard
alisema mkutano huo ni kama kichocheo cha mabadiliko.
"Ngarama za
Matibabu kwa Wagonjwa wa Kisukari ni kubwa, Mfuko wa kusaidia Wagonjwa wa
Kisukari Duniani ulianzishwa mwaka 2002, kwa maono ya kusaidia watu wanaoishi
na ugonjwa huo katika nchi zinazoendelea," anasema Anders Dejgaard.
"Tumekuwa
tukisaidia kuzuia ugonjwa wa kisukari na upatikanaji wa huduma kwa watu
walioathirika na ugonjwa huo katika ukanda wa Afrika tangu kuanzishwa kwa Mfuko
huu. Leo, zaidi ya muongo mmoja amepita na mipango yetu imeonyesha matunda
makubwa, shukrani kwa juhudi za pamoja za mabingwa wa ndani ya Nchi husika,
washirika wa ndani ni muhimu katika kufikisha msaada wa huduma. Pengine
ushiriki wa Prof Ayoub Magimba, Wizara ya Afya, Tanzania anaweza kuzungumzia
kuhusu maendeleo makubwa ya Tanzania ndani ya eneo la huduma ya kisukari ya
zaidi ya miaka 10-15 iliyopita," amesema Dkt Anders Dejgaard.“
Mikutano huo
unalenga kutatua matatizo yanayoambatana na Kisukari unalooendela kukua barani
Afrika kwa sasa ambao umeonekana kukua mara tatu zaidi ndani ya miaka mitano
iliyopita.
Dk. Kaushik alisema
kuwa, mbali na mjadala wa uchunguzi wa kisayansi, Mambo mengine yatakayo
jadiliwa ni pamoja na
• Kuongezeka kwa
ugonjwa wa kisukari katika nchi zinazoendelea, na lengo hasa juu Africa na
namna ya kutatua matatizo yatokanayo.
• Kujadili kuhusu
mzigo wa kijamii na kiuchumi unaotokana na watu wenye ugonjwa wa kisukari ,
familia zao na jamii kwa ujumla.
• Umuhimu wa
kutafuta ufumbuzi wa Ugonjwa huu.
• Taarifa za
uchunguzi za wataalam ngazi za mkoa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni