Zinazobamba

UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA: WANAHARAKATI WAMJIA JUU RAIS MAGUFULI


Mtandao wa Wanawake wa Katiba na Uchaguzi, umemuomba Rais John Magufuli kusimamia kikamilifu utekelezwaji wa mikataba iliyosainiwa na Tanzania katika usawa wa kijinsia ili kupunguza pengo lililopo kuelekea usawa wa 50/50 katika nafasi za uongozi.

Maombi hayo yamekuja kufuatia uteuzi wa wakuu wa mikoa uliofanywa mwishoni mwa wiki iliyopita na wanawake waliopenya kuwa ni watano kati ya wateule 26, ikiwa ni sawa na asilimia 20.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia (TGNP), Gloria Shechambo ilielezea kuwapo kwa dalili za kuwakandamiza wanawake kutokana na idadi ndogo ya wanaoteuliwa kushika uongozi katika ngazi za uamuzi.

Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi aliwahi kusema kuna makatibu wakuu wa wizara mbalimbali na manaibu wao 50, huku wanaume wakiwa 40 sawa na asilimia 80.

Hakuna maoni