MKUU MKOA WA DAR AWAKOMALIA WALIOBOMOLEWA,SOMA HAPO KUJUA
Said Mecky Sadick, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
SERIKALI imegoma kuwapa viwanja wananchi
waliobomolewa nyumba zao zilizokuwa bondeni kwa madai jiji limejaa na hakuna
viwanja,
Said Mecky Sadick, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es Salaam.
Hivi
karibuni serikali iliendesha bomoabomoa kwenye maeneo ya bondeni hususan katika
Mbonde la Mkwajuni na kusababisha vifo na mateso kwa baadhi ya wakazi hao.
Bona
Kaluwa, Mbunge wa Jimbo la Segerea na Abdallah Mtulia Mbunge wa Jimbo la
Kinondoni, walizuia kuendelea kwa bomoabomoa hiyo kupitia Mahakama.
“Wakazi
wa Kinondoni waache jeuri, wanajua fika kuwa wamejenga sehemu zisizostahili,
wamebomolewa lakini wamerudisha vibanda na kuendelea kuishi na kusema serikali
inawaonea,” amesema Sadick na kuongeza;
“Serikali
haiwezi kuwapa ardhi waliobolewa, kwanza ardhi hakuna katika Jiji la Dar es
Salaam, halafu unamsaidiaje mtu aliyevunja kisheria?” amesema.
Sadick
amesema kuwa, serikali haikuwapeleka maeneo hayo na kwamba haina sababu ya
kuingia gharama kuwapa viwanja.
Katika
mkutano huo Bona aliitaka serikali kuwapa viwanja waathirika kama ilivyofanya
mwaka 2012 ambapo wananchi walipewa viwanja Mabwepande.
“Serikali
ilichangia kuongeza kasi ya ujenzi wa mabondeni sababu, ili ruhusu huduma za
kijamii kupelekwa katika maeneo hayo kama shule, barabara na hospitali na
iliwapa moyo kuendelea kujenga katika maeneo hayo,” amesema Bona.
Mtolea
amesema kuwa, wananchi waliojenga vibanda katika Bonde la Mkwajuni siyo jeuri
kama alivyosema Sadick na kwamba hali ngumu ya maisha ndiyo iliyosababisha
kujenga eneo hilo.
“Waliojenga
vibanda siyo jeuri, hali ngumu ya maisha ndiyo inayosababisha wasihame
kwasababu hawana mahali pa kwenda,” amesema Mtulia.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni