GAZETI LA DIRAMTANZANIA LAZIDI FUKUZISHA KAZI VIGOGO,BAADA YA KUMWONDOA BALOZI SEFUE SASA LAMWONDOA KIGOGO HUYU,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
GAZETI la DiraMtanzania LA Jumatatu ya tarehe 07/03/2016 toleo no.405 ,kufichua madudu
ya Katibu mkuu mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) Dk Primus
Nkwera kuwa hana sifa ya kuongoza Idara hiyo baada ya kubainika amefoji shahada
yake ya tatu yaani PHD,
Hatimaye DKT Nkwera amejiuzulua nafasi hiyo
ailiyokuwa nayo.
Uamuzi wa kujiuzulu kwa Dr. Nkwera ulitangazwa
katika ofisi kuu za Baraza hilo zilizopo
Mikocheni Dar es Salaam juzi na Mwenyekiti wa Bodi,Mhandisi
Steven Mlote na kusababisha baadhi ya wafanyakazi
kuangua kilio.
Akizungumza katika kikao cha dharura cha wafanyakazi wote wa
baraza hilo,Mlote alisema Dr. Nkwera amejiuzulu ili kulinda
hadhi ya Nacte kutokana na habari iliyoandikwa na Gazeti la
Dira ikimtuhumu mambo mbalimbali.
Mlote alisema kwa mujibu wa Dr. Nkwera, nafasi hiyo haipaswi
kushikwa na mtu mwenye tuhuma ya aina yoyote, na ametafakari
na kuona ajiweke kando na uongozi wa Nacte ili uchunguzi ufanyike akiwa
pembeni.
"Tumetumia muda mwingi kutafakari hoja ya Dr.
Nkwera na hatimaye tumekubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande," alisema Mlote na kuongeza:
"Kazi kubwa iliyofanywa na Dr. Nkwera akiwa kiongozi wa
Nacte inafahamika na kila mmoja, vilio na machozi ya wafanyakazi wenzake
yanadhihirisha kuwa kujiuzulu kwake kunaacha simanzi kubwa.
"Najua mmepata mshtuko mkubwa, lakini Dr Nkwera hajafa,
yuko hai na huyu bado ni mtumishi wa serikali. Alichofanya ni kuamua kuachana
na ukatibu utendaji.
"Tutaendelea kumtumia itakapobidi kwa ushauri.Wakati
mwingine lazima mkubaliane na hali hii, lakini pia
endeleen kuchapakazi kwa ufanisi kama kawaida kana kwamba bado mko na Dr.
Nkwera."
Kutokana na kujiuzulu kwake, Mlote alisema
bodi imemteua Mkurugenzi wa Mitaala wa Nacte, Dr Adolf Rutayunga kukaimu nafasi
hiyo wakati taratibu nyingine zikiendelea.
Akizungumza na wafanyakazi hao, Dr. Rutayunga alisema viatu
alivyoviacha Dr. Nkwera ni vikubwa kwake, lakini akaahidi kuendeleza
yote aliyoyaacha.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni