FREEMAN MBOWE AMALIZA UBISHI KWA LOWASSA,ATOBOA SIRI NZITO,SOMA HAPO KUJUA
FREEMAN Mbowe,
Mwenyekiti wa Chadema-Taifa amesema, Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea wa chama
hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuungwa mkono na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), hakutoa hata senti moja alipojiunga na chama hicho, anaandika Happyness Lidwino.
Mbowe amezungumza hayo kwenye Mkutano wa
Baraza Kuu la Chadema linaloendelea kwa sasa Jijini Mwanza.
Amesema kuwa, pamoja na kuwepo kwa kauli nyingi kwamba, Lowassa
alimmwaga pesa kabla ya kujiunga na chama hicho, ukweli unabaki kuwa hakutoa
pesa yoyote kama ilivyokuwa ikidaiwa.
“Watoto wangu walikuwa wanakula sana maharage, sasa siku moja
wakala nyama, jirani akasema umeona Lowassa kaja Chadema,” amesema Mbowe.
Akizungumzia migogoro ya kichama iliyokuwa imejitokeza kwenye
uchaguzi uliopita Oktoba 25 mwaka huu Mbowe amesema, kuna kila sababu
kushughulikia migogoro hiyo kwa haraka.
“Migogoro mingi ndani ya Chadema imepelekea kuanguka kwa chama,
hivyo itashugulikiwa kwa haraka,” amesema na kuongeza;
“Uchaguzi mkuu wa chama ni Oktoba 2018.”
Amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, harakati za kisiasa
hasa kukikuza chama ni gharama kubwa jambo ambalo chama kinajitahidi
linakabiliana nalo.
Amesema kwamba, pamoja na mambo yote ndani ya chama hicho lakini
suala la rushwa haliwezi kuvumiliwa hata mara moja.
Akifafanua kauli hiyo amesema kwamba, Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kimeishi kwa kulea rushwa na kwamba, hali hiyo ndio imekifikisha hapo kilipo
sasa.
Amesema, hali hiyo inaelekea kuingia Chadema jambo ambalo
linaweza kusababisha kupasuka kwa chama hicho endapo halitashuhulikiwa.
“Jambo ambalo hatutalivumia ndani ya Chadema ni swala la rushwa
kwani rushwa linagawa taifa, sasa swala la rushwa lililelewa na CCM na sasa
inataka kuingia Chadema,” amesema.
“Kuna majimbo kama Iringa, Rukwa, Arusha Chadema waliachiwa kwa
asilimia mia moja na Ukawa lakini kwanini wameshindwa kuchukua ushindi wa
kutosha katika majimbo hayo?” amehoji.
Akizungumzia changamoto za Ukawa Mbowe amekiri kuwepo na kwamba,
hakuna sababu ya kuzikwepa.
“Changamoto zilizopo ndani ya Ukawa hakuna haja ya kuzikimbia
bali ni kupambana nazo,” amesema.
Akizungumzia
umoja wa kimataifa amesema kwamba, Chadema hakikubaliani na mtu yoyote
anayetaka ama kushabikia kauli za kuligawa taifa.
“Nawashauri tunapokuwa popote lazima tukatae nchi yetu kugawa
vipande vipande. Hatukotayari kufanya kosa kama hilo wala kushabikia kuligawa
taifa ,” amesema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni