CHADEMA - HII NDIO SURA YA RAIS MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
RAIS John Magufuli anatajwa kuwa mtawala
anayeendekeza kisasi cha kiutawala kwa wananchi walioamua kupigia kura vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anaandika Regina Mkonde.
Jana wakati Rais Magufuli
akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi namba
mbili alisema, “huwezi ukapeleka chakula kwa mtoto wa jirani” kauli ambayo
imeeleza kuwa ya kibaguzi.
Kauli
hiyo imetafsiriwa na Ukawa kwamba Rais Magufuli anaonekana kutokuwa tayari
kushirikiana na vyama hivyo (jirani) licha ya kuwa ndio walio wengi katika
kuwawakilisha wananchi jijini Dar es Salaam.
Kauli
hiyo pia imejadiliwa kwa upana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kuwa na
ukakasi uliotoa tafsiri mbalimbali.
Charles
Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala amesema, kauli hiyo imelenga
kuwaponda viongozi wa upinzani na kwamba, inaleta picha mbaya katika ulimwengu
wa demokrasia nchini.
“Kauli
yake imelenga kuuponda upinzani, licha ya hayo kampeni zimeisha, hakuwa na
sababu ya kuongea kauli hiyo mbele ya wananchi katika shughuli za kitaifa
ambazo hazilengi itikadi za kisiasa,” amesema Kuyeko.
Amesema
kuwa, huu si wakati wa kujadili tofauti za itikadi za vyama bali ni wakati wa
kutatua changamoto za wananchi.
Boniface
Jacob, Meya wa Manispaa ya Kinondoni amesema kuwa, hata kama rais ataitekeleza
kauli yake, haitaathiri maendeleo ya halmashauri yake kwasababu mapato yake
yanakidhi mahitaji yake.
“Kwa
upande wangu kauli yake haitaniathiri kwasababu Kinondoni tunajiweza
hatutegemei sana msaada kutoka serikali kuu. Kinondoni ina uwezo wa kukusanya
mapato ya kiasi cha bilioni 50 kwa mwaka,” amesema Jacob.
Amesema,
Kinondoni ina vyanzo vingi vya mapato, ambapo mapato yake yanatosha kutekeleza
ahadi zake ikiwemo uboreshaji wa miundombinu na huduma za kijamii.
“Hata
kama atajaribu kutuwekea vikwazo ili tushindwe tekeleza ahadi zetu na kuonekana
hatufai mbele ya wananchi, hatofanikiwa, tutatekeleza ahadi zetu na wananchi
watashuhudia mabadiliko ya uongozi wa UKAWA.
Pia
amenukuliwa akisema, “nawapongeza wakazi wa Kinyerezi kwa kunichagulia mbunge
anayetoka kwenye chama changu, nawahakikishieni kama kuna changamoto za Jimbo
la Segerea nitazipa kipaumbele katika utatuzi wake.”
Licha
ya hayo, Magufuli amesema aliamua kumchagua Paulo Makonda aliyekuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la
kuwanyamazisha maadui zake.
“Hata
Makonda nimemuacha Dar es Salaam ili wabaya wake wamuone akipanda cheo, wenye
chuki wajinyonge zaidi,” amenukuliwa Rais Magufuli
Hakuna maoni
Chapisha Maoni