BALOZI MWAPACHU AIPASUA CCM,MAKADA WAIBUKA NA KUTAKA AFUKUZWE HARAKA SANA,DHAMBI YA USARITI KUMTESA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SIKU chache
kupita baada ya Balozi Juma Mwapachu kutangaza kurudi rasmi katika Chama cha
Mapinduzi CCM kwa madai kuwa biashara
zake haziendi vizuri kutokana yeye kuwepo kwenye vyama vya upinzania,
Nalo shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu nchini
ambao ni wanachama wa chama cha CCM wameibuka
nakukitaka chama chao kumfukuza mara moja Balozi Mwapachu kwa kile
wanachodai ni msariti.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini
Dar es Salaam,Katibu Hamasa wa Shirikisho hilo, Mganywa Nzota amesema Kitendo
cha Balozi Mwapachu kutangaza kurudi CCM kwa hoja ya biashara zake aziende
vizuri ni suala linalokichafua chama hicho,
“Balozi Mwapachu amekivua nguo chama pale anaposema biashara zake haziendi vuzuri kutoka na yeye kuwepo upizani ni kuonyesha
chama chetu kinalinda wakwepa kodi ambao wamekuwa wakiikosesha mapato serikali
wakati jambo hilo sio kweli kwani sasa serikali ya Magufuli inapambana na
wakwepa kodi,kwahiyo Balozi Mwapachu amechafua chama”amesema Nzota,
Nzota amesema licha ya kukichafua chama pia Balozi
Mwapachu amekiuka katiba ya CCM ya mwaka 1977 na toleo la mwaka 2012 ibara ya
tano kifungu kidogo cha kwanza kinaleza malengo ya msingi kushika dola,huku
akisema Balozi Mwapachu kwa kauli zake wakati akihama chama hicho alitoa kauli
ambazo zingeweza kusababisha chama kishindwe uchaguzi,
Nzota amesema kwa hoja hizo chama hakitakiwa hata
kidogo kuendelea kuwa na Mwanachama huyo kubaki na kadi ya chama.
“Kwa mantiki hii kupokelewa kwake kimekifedhehesha
chama na kukidhalilisha sana chama chetu tunakitaka kamati ya siasa ya
Kinondoni kuwachukulia hatua kali viongozi wa CCM kata ya Mikocheni kwa hatua
ya kumpokea Balozi Mwapachu”amesema Nzota.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni