Zinazobamba

WAZIRI NAPE NAYE ATUMBUA MAJIPU BMT,SOMA HAPO KUJUA


Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari leo hii katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mtendaji mkuu wa baraza ilo Bw. Henry Lihaya (wa kwanza kushoto) leo jijini Dar es Salaam kutokana utendaji usiolizisha. Picha na Daudi Manongi.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Mhe. Nnauye ametengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo.

“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,”alisema Mhe. Nnauye.

Aliongeza kwa kusema kuwa, miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.

Kutokana na utenguzi huo Mhe. Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.

Vilevile, Mhe. Nnauye amemtaka mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo nchini.

Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani
  
BAADA YA NAPE KUTUMBUA JIPU HILO MRITHI WA ALIYETUMBULIWA JIPU HILO HUYU HAPA



Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Deonis Malinzi amemteua Mohamed Kiganja kuwa Katibu Mtendaji mpya wa baraza hilo baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Bw. Henry Lihaya kutenguliwa.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Malinzi ameeleza kuwa uteuzi huo umekuja baada ya kuona mapungufu ya utendaji kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.
“Baraza la Michezo Tanzania limefikia maamuzi haya baada ya kutoridhishwa na utendaji wa Bw. Lihaya na hivyo Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kufanya maamuzi ya kumtengua” alisema Bw. Malinzi
Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya BMT namba 12 ya mwaka 1967 kifungu namba 5(1) ambacho kinampa mamlaka Mwenyekiti wa BMT kuteua Katibu Mtendaji baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana.
Aidha kabla ya uteuzi huo Kiganja alikuwani Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka 2015 mpaka uteuzi wake ulivyofanyika.
Pia aliwahi kufanya kazi kama Afisa Mwandamizi Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania na Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi wa Waziri Mkuu, anashahada ya kwanza ya Elimu katika masuala ya Michezo na Utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Hakuna maoni