TANZANIA IPO HATARINI KUJWA JANGWA,NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA ATOA TAHADHARI NZITO,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni NAIBU waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.Luhaga Mpina |
IMEELEZWA kuwa asilimia 60 ya meneo ya nchi yapo
hatarini kugeuka Jangwa kutokana kukithili vitendo vya uharibifu wa
Mazingira.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo,
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na
NAIBU waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.Luhaga Mpina
wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia siku ya
Mazingira duniani ambayo inaadhimishwa kila mwaka siku ya 3 Marchi,
Ambapo Amesema
kwa sasa kutokana na taasisi mbali mbali kutozingatia maelekezo ya sheria na
kuendesha shughuli zisizoendelevo na kusababisha kuongezeka kwa kasi uharibifu
wa mazingira jambo analosema litaipeleka nchi kuwa jangwa,
Amesema kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la
watu wanaofanya vitendo vya ukataji miti
kwa kasi na bila kuzingatia athari za taifa kwa baadae,
Mpina ameitaja mikoa ambayo ipo mbioni kuwa
jangwa ni
Simiyu,Mwanza,ShinyangamSingida,Dodoma na Kilimanjaro ambapo amedai uharibifu
wa Mazingira umechangia kuwepo kwa ukame wa kutisha na upungufu mkubwa wa
Chakula kila mwaka,
Amebainisha kuwa Hali hiyo pia imechangiwa kwa kiasi
kikubwa na uharibifu wa misitu na matumizi ya Ardhi ambapo ametolea mfano kwa
kusema Tanzania inapoteza hekta 400,000 za misitu kila mwaka kutokana na
ukataji miti hovyo kwa ajili ya kilimo pamoja na matumizi ya makubwa ya
nisharti ya kuni na mkaa,
Aidha,Mpina ametumia nafasi hiyo kuzitaka
Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanahifadhi mazingiri na kusimamia sheria
husika ili kuweza kulikoa Taifa na hatari ya kuwa jangwa,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni