SHEIKH PONDA NAYE AIBUKA SASA NA KULIKAANGA BAKWATA, NI KUHUSU SAKATA LA ZANZIBAR,,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita baada ya Baraza la Waislam
nchini,(BAKWATA) kuuunga mkono marudio ya uchaguzi visiwani Zanzibar, naye
KIONGOZI wa
Jumuiya na Taasisi za Kislam nchini,Sheikh Ponda Issah Ponda aimeibuka na
kupinga marudio ya uchaguzi huo, kwa madai kuwa uchaguzi huo utawagawa wananchi visiwani humo,
Hata hivyo Sheikh Ponda amekanusha vikali kuhusu juu
ya uwepo wa barua iliyoandikwa na kiongozi wa jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmad
kwenda kwa Sheikh Mkuu mkoani Dar es Salaam,Sheikh Alhad Mussa Salum kuhusu
kuunga mkono marudio ya uchaguzi visiwani Zanzibar.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo kwenye msikiti wa kichangani jijini Dar es Salaam,Sheikh Ponda amesema Jumuiya
hiyo inaamamini uchaguzi uliofanyika octoba 25 mwaka jana ulikuwa huru na wa haki.
“Uchaguzi
huru na wa haki ulishafanyika octoba 25 mwaka jana,kwani Wazanzibar walitumia
haki yao ya msingi kuwachagua viongozi
wanaowataka,na sisi hatuoni kosa lilofanywa mpaka uchaguzi ule kufutwa,”
“Ndio maana
tunasema hatukubaliani na marudio ya uchaguzi ,marudio haya ya uchaguzi
yataleta mgawanyiko mkubwa visiwani Zanzibar na kurudisha nyuma maendeleo”amesema
Sheikh Ponda.
Sheikh Ponda
amefafanua kuhusu barua ya Sheikh Farid kwa kusema kuwa anauhakika kuwa hakuna
barua iliyoandikwa.
“Hakuna
barua hiyo,na hizo ni habari za kuzusha tu kwani Sheikh Farid niliongea nae
amenihakikishia kuwa aungani na kinachoendelea visiwani Zanzibar cha kurudiwa
uchaguzi”Amesema Sheikh Ponda.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni