SAKATA LA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR,WANAHARAKATI WA LHRC WAIBUKA NA KUMVAA JECHA WA ZEC,SOMA HAPO KUJUA
Na Exaud Mtei (Msaka Habari)
Zikiwa
zimesalia Takribani siku 18 kufanyika kwa marusio ya uchaguzi mkuu wa marudio
visiwani Zanzibar,kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wameibuka na kupina
uchaguzi huo huku wakimtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Zanzibar JECHA
SALUM JECHA kujiuzulu mara moja kwa kushinda kusimamia uchaguzi wa zanzibar na
kusababisha kuvurugika kwa uchaguzi huo.
Katika mkutano na waandishi wa habari mapema
leo kaimu mkurugenzi wa LHRC Bi IMELDA LULU URIO amesema kuwa hatua ya
mwenyekiti JECHA kufuta uchaguzi bila kufuata sheria kunampunguzia sifa za
kuongoza tume hiyo na ni kiashiria cha wananchi kukosa imani naye hivyo
anatakiwa kuchukua hatua ya kujiondoa
Wakili HAMIS MKINDI kutoka LHRC |
.
Amesema kuwa kufutwa na kutangazwa upya kwa
uchaguzi wa Zanzibarkunakiuka
katiba,sheria,na kanuni za uchaguzi na pia misingi ya democrasia misingi ya
utawala na sheria nchini.
Amesema kuwa katiba ya Zanzibar na sheria za uchaguzi hazijampa mamlaka
mwenyekiti na hata tume yote kufuta uchaguzi na hivyo kilichotokea Zanzibarkimeaacha watanzania wakiwa hawaelewi
ni sheria na katiba ipi imetumika kufanya swala hilo.
Wanahabari wakidaka Taarifa hiyo |
“kwa mujibu wa kifungu cha 88 cha sheria ya
uchaguzi zanizbar wasimamizi wa uchaguzi ndio wenye mamlaka ya kutangaza
matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani,jambo
ambalo wasimamizi wa uchaguzi walishalifanya kwenye majimbo mengi ya uchaguzi
kwa kuwatangaza washindi na kuwapatia vyeti kudhibitisha uhalali wao hivyo
tunashangaa uchaguzi ulianza kuonekana sio halali wapi”amehoji wakili huyo
msomi Kutoka LHRC
Bi IMELDA ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu
cha 123 cha sheria ya uchaguzi Zanzibar mtu
akishachaguliwa uchaguzi wake hautohojiwa isipokuwa kwa kupeleka shauri
mahakamani,hivyo kwa msingi huo LHRC wanaona kwamba hakuna kifungu chochote cha
sheria kinachoipa tume ya uchaguzi au mwenyekiti wake mamlaka ya kufuta
uchaguzi na kuamuru marudio isipokuwa kwa amri ya mahakama.
Aidha katika hatua nyngine LHRC wamehoji
kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea yakiwahusisha wakuu wa nchi akiwemo
Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DR JOHN POMBE MAGUFULI,Raisi wa
Zanzibar DR ALLY MOHAMED SHEIN,Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh seif
sharif Hamad,pamoja na marais wastaafu wa Tanzania ambapo wamesema kumekuwa na
ukimya mkubwa baada ya yale mazungumzo ambapo watanzania hawakupewa taarifa
halisi kuwa nini hasa kilikuwa kinazungumzwa katika mazungumzo hayo huku
akisema wananchi wana haki ya kufahamu kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
Matokeo
ya uchaguzi wa Zanzibar yalifutwa Rasmi
na mwenyeiki wa tume ya uchaguzi wa Zanzibar JECHA SALUM JECHA kwa sababu kuwa
kulikuwa na dosari kadhaa ambapo uchaguzi huo sasa utafanyika tarehe 20 mwezi
wa pili huku chama cha wananchi CUF wakiwa tayari wameshajiondoa katika
uchaguzi huo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni