NCHI YAZIDI TAFUNWA KWA UFISADI,MABILIONI YAIBWA NSSF,KAMPUNI YA MALINZI WA TFF YAHUSIKA,SOMA HAPO KUJUA
Profesa Samweli Wangwe, Mwenyekiti wa NIP |
BODI ya
Wakurugenzi ya Shirika la Tija la Taifa (NIP) imeishauri serikali kuunda tume
ya kuchunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali zaidi ya dola za Kimarekani
1.5 bilioni, anaandika Josephat Isango.
Kwa
mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya mwaka 2012/13,
imebaini kiasi cha dola za kimarekani 1,532,458.91 zilizotolewa na Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) zimetumika kinyume na taratibu za kisheria.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Samweli Wangwe, Mwenyekiti wa NIP, amesema
kuwa, fedha hizo zilikua za mkopo kwa ajili ya uendelezaji wa jengo
la Maarifa lililopo mtaa wa Ohio na Hollis jijini Dar es Salaam ambalo
linamilikiwa na Shirika hilo zilipo.
Amesema, ripoti hiyo
ilionyesha kuwa, kiasi cha dola za kimarekani 480,000 zilitumika kuilipa
kampuni ya Zawadi Communication Limited ambayo inamilikiwa na Jamal Malinzi
ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), kama gharama za udalali
wa kuitafutia NIP mbia wa ujenzi wa jengo hilo ambao ni NSSF.
Ameongeza kuwa,
mashirika hayo mawili ni mali ya serikali, hivyo basi hakukuwa na ulazima wa
kumtafuta dalali wakati makatibu wakuu wangeweza kukaa pamoja na kujadiliana
namna ya kuweza kuingia makubaliano ya mkopo huo.
Amesema, licha ya
kufanyika kwa malipo hayo, lakini ripoti hiyo imeonyesha kuwa, NIP haikuitisha
zabuni yoyote ya kutafuta kampuni ya udalali ya kutafuta mbia, jambo ambalo ni
kinyume na sheria.
Alisema Kutokana
na hali hiyo, bodi hiyo ilipata mashaka juu ya malipo hayo na kuitaka serikali
kuchunguza mwenendo mzima wa malipo hayo kama ulifuata taratibu za kisheria.
“NIP haikutangaza
zabuni yoyote ya kutafuta kampuni ya udalali kwa ajili ya kutafuta mbia,lakini
malipo yameonyesha kuwa, kampuni hiyo ililipwa kiasi hicho Juni16 mwaka
2011,jambo ambalo ni kinyume na sheria,” amesema Profesa Wangwe.
Amesema, licha ya
malipo hayo kufanyika, lakini pia kiasi cha dola 831,214.48 zimebainika
kutumika kinyume na sheria wakati ujenzi wa jengo hilo haujaanza kinyume na
makubaliano ya mkataba wa mkopo huo.
Wangwe aiwambia
waandishi kuwa bodi hiyo pia ilibaini kuwa, fedha zote ambazo ni dola
1,532,458,91 ziliingizwa Katika akaunti ya NIP kwa mkupuo moja wakati
makubaliano yalikuwa ni kuingiza kwa awamu kulingana na mahitaji halisi.
“Kutokana na
hali hiyo, NIP inatakiwa kulipa jumla ya dola 1,002,228.13 ambayo ni pamoja na
riba ya asilimia 13.08 kwa kipindi chote cha miaka mitano, jambo ambalo
linazidi kuitia hasara serikali,” amesema.
Alifafanua
kuwa, mpaka sasa shirika hilo halina vyombo vya usafiri, badala yake viongozi
wakuu akiwamo Mkurugenzi anakodisha gari lake binafsi kwa ajili ya matumizi ya
ofisi.
Profesa Wangwe amesema kuwa, licha mkataba huo kuonyesha
matumizi ya fedha hizo ambayo ni pamoja na kulipa gharama za wapangaji za
kutafuta sehemu nyingine ili kupisha ujenzi huo pamoja na NIP kukodi ofisi
wakati ujenzi huo unaendelea, lakini fedha hizo zimetumika kinyume na
makusudio.
Amesema baada
ya kubaini upungufu huo, bodi hiyo iliitisha kikao cha dharura kwa ajili ya
kuzungumza na menejimenti kuhusu suala hilo ambao na wenyewe walikiri kukiukwa
kwa makubaliano ya mkataba huo kwenye matumizi ya fedha hizo.
Wangwe amesema kutokana na hali hiyo, bodi hiyo iliwasilisha
mapendekezo ya kuitaka serikali kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Shirika hilo,
Joel Mlanzi ambaye tayari ameshasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa suala
hilo.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni