Zinazobamba

MUSEVENI WA UGANDA MATATANI,SOMA HAPO KUJUA

Dk. Kizza Besigye, mgombea urais kupitia Chama cha Forum for Democratic Change
Dk. Kizza Besigye, mgombea urais kupitia Chama cha Forum for Democratic Change


CHAMA tawala cha NRM nchini Uganda kinachowakilishwa na Rais Yoweri Museveni katika ngazi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana, kimeanza kunyooshewa kidole kwa madai ya kushirikiana na serikali kuiba kura.
Tetesi za wizi wa kura zilisababisha Dk. Kizza Besigye, mgombea urais kupitia Chama cha Forum for Democratic Change kufuatilia mahali ambapo wizi huo ulidaiwa kufanyika na baadaye alijikuta akikamatwa na polisi kisha kupelekwa kusikojulikana.
Hata hivyo, baada ya saa nane kukamatwa kwa Dk. Besigye, Ssemujju Ibrahim Nganda, msemaji wa chama hicho alisema kuwa, mgombea huyo wa urais alichiwa na polisi.
Kanali huyo mstaafu ambaye ni kigogo wa upinzani nchini Uganda alikuwa amekamatwa katika kitongoji cha Naguru, mjini Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.
Wafuasi wa upinzani, wakiambatana na kanali Besigye, wanadai walifumania watu wakiiba kura na wakataka usaidizi wa polisi kukagua nyumba hiyo lakini wakazuiliwa.
Besigye alikamatwa na maafisa wa polisi walioondoka naye kutoka eneo hilo na baadaye kuachwa.

Hakuna maoni