MEYA WA UKAWA KINONDONI,APEWA RUNGU NA CHADEMA,SOMA HAPO KUJUA
Boniface Jacob, Meya wa Halmashauri ya Kinondoni |
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo kimemkabidhi Ilani Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob ili imuongoze katika utendaji wake.
Akikabidhi
ilani hiyo katika Ofisi za Manispaa kwa niaba ya chama, Mratibu wa Chadema
Kanda ya Pwani, Kasmil Mabina amesema, anamkabidhi meya ili aweze kutekeleza
ahadi za Chadema kwa wananchi kwa kuwa yeye ndiye muwakilishi wao.
Ilani hiyo
imeorodhesha vipaumbele vya chama ikiwa ni pamoja na kushuhulikia suala la
bomoabomoa, maji, elimu. Pia Chadema kimemtaka kuwaagiza madiwani kufuatilia na
kuhakikisha waliobomolewa wanapata haki zao ikiwemo kulipwa fidia.
Mabina akisoma
Ilani hiyo amesema, Jacob pia anajukumu la kushugulikia elimu katika Manispaa
yake na kuhakikisha anakusanya mapato ya kutosha kama chama kilivyokuwa
kinaahidi.
“Inatakiwa
tujitahidi ili tuoneshe mfano kwa CCM na tuwaaminishe wananchi kwamba upinzani
pia unaweza kuongoza vizuri. Ilani hii tuliyompa Jacob imetokana na katiba ya
chama inayomtaka Meya na Madiwani kuisimamia manispaa na kuanda mipango kazi
yake na kuwasilisha utekelezaji wake katika kikao kikuu cha chama,” amesema
Mabina.
Jacob baada ya
kukabidhiwa Ilani hiyo ameahidi kutekeleza yote aliyoagizwa na chama chake huku
akiwataka wananchi kuendelea kumuamini katika utendaji wake.
“Nataka niwatoe
hofu wananchi wangu kwamba, kukabidhiwa Ilani ya chama haimaanishi kwamba
nitakuwa Meya wa wana Chadema au Ukawa tu, bali nitayachukuwa mazuri yote kwa
ajili ya manufaa ya wananchi wote,” amesema
Ameandika Sarafina Lidwino.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni