MCHUNGAJI MSIGWA NI MOTO WA KUOTEA MBALI,AMBWAGA MWAKALEBELA,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali kesi
ya kupinga matokeo yaliyompa Ubunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
(Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake kwenye Uchaguzi huo,
Frederick Mwakalebela (CCM).
Mahakama hiyo pia imeamuru Mwakalebela kumlipa
Mchungaji Msigwa gharama za kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana na kupata
usajili wa mahakama hiyo Novemba 30.
“Kesi ya mwakalebela yatupwa anatakiwa kulipa
gharama. Nikiwa na wakili wangu msomi Jane Masey,” Mchungaji Msigwa ameandika
kwenye ukurasa wake wa Facebook akiambatanisha picha yake na Wakili wake.
Katika shauri la msingi la kesi hiyo namba 5 ya
mwaka 2015 ya kupinga matoke, Mwakalebela aliwatuhumu Mchungaji Peter Msigwa na
msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini, Ahmed Sawa kwa kukiuka sheria
na taratibu za uchaguzi hali iliyopelekea yeye kupata matokeo mabaya yasiyo
halali
Hakuna maoni
Chapisha Maoni