CHADEMA YAMUONYA RAIS MAGUFULI,NI KUHUSU UCHAGUZI WA UMEYA WA JIJI LA DAR,SOMA HAPO KUJUZ
Mratibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Casmir Mabina akimkabidhi Ilani ya Chadema/Ukawa Meya wa Ilala, Charles Kuyeko |
NA KAROLI VINSENT
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kimemtaka Rais John Magufuli kuaacha kuingilia uchaguzi wa Meya mkoani Dar es
Salaam kwa madai kuwa anaingilia uhuru wa wananchi waliofanya kuwachagua
madiwani wao.
Hayo yameelezwa leo jijini dare s Salaam na Mratibu
wa Kanda ya Pwani ya Chama hicho,Casmir Mabina wakati alipokuwa akimkabidhi
ilani ya Chama hicho ambayo iliyotumika wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 kwa
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini
hapa,Charles Kuyeto,
Ambapo Mabina amesema Mgogoro unaoendelea sasa wa kutaka kukwamisha
uchaguzi wa Meya jijini hapa unatokana na busara za moja kwa moja za Rais
Magufuli kwa kutumia madaraka yake kukwamisha uchaguzi huo,
Amesema Kitendo cha kuwaruhusu wabunge wa Viti
Maalum kutoka Zanzibar kuja kupiga kura kwenye uchaguzi wa Meya ni kitendo
anachodai hakikubaliki na kinafaa kupigwa vita na kila mmoja,
Amezidi dai kuwa lawama kwa Rais Magufuli zinatokana
na kitendo cha kumfumbia Waziri wa Tamisemi Goergy Simbachawene kuendeleza
kumpangia mkurugenzi wa Jiji Wabunge hao anaowaita ni mamluki.
Mabina ametoa tahadhari kwa Rais Magufuli kwa
kumtaka kuliacha suala hilo liamuliwa na Madiwani wa wananchi waliowachagua kwa
kura,huku akisema kitendo chake cha kuingilia mgogoro huo kutaweza wagawa
wananchi na hata hiyo anayodai kasi ya kutumbua majibu itaonekana ni kazi bure,
Kwa Upande wake Meya Kuyeto amempongeza kiongozi
wake huyo wa chama aliyemkabidhi ilani hiyo huku akidai vipaumbele vyote vya
Ilani vilivyotumika wakati wa Kampeni ikiwemo kipaumbele cha elimu ,akisema ni
wakati wakutekeleza kwa vitendo,
Amesema kwa sasa wameshapata vyanzo vya mapato katika manispaaa hiyo,ambavyo amedai fedha
hizo zinatachangia katika kuboresha miundombinu katika Halmashauri ya Ilala
ambayo anaiongoza,
Meya huyo ameongeza kuwa kwa sasa tangu aingie
ameshuhudia hali mbaya katika shule za Halmashauri yake ikiwemko mazingira mabovu
ya kusomea pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa huku akijitabainisha kuwa
watahakikisha wanapambana navyo katika kipindi kifupi ili wananchi wafurahie
uongozi wa ukawa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni