HOSPITALI YA UPASUAJI YAZINDULIWA TABATA KISUKULU,NI YA JPM,SOMA HAPO KUJUA
Pichani wa kwanza kushoto ni Msaidizi wa mganga mkuu wa wilaya ya ilala,Dkt Willy Sangua akijaindaa kukata utepe kwenye uzinduzi wa hospitali ya upasuaji maeneo ya Tabata kisukulu |
Sehemu za mashine za kisasa za upasuaji akionyeshwa mgeni rasmi |
TAASISI ya JPM imezindua Hospitali ya upasuaji na
yenye kutoa
huduma mbali mbali , maeneo ya Tabata Kisukulu Jijini dare s Salaam
ambayo itakuwa inatoa tiba kwenye magonjwa yote yanaitajika kufanyiwa upasuaji.
Akizundua Hospitali hiyo,Msaidizi wa mganga mkuu wa
wilaya ya ilala,Dkt Willy Sangua amesema Hopsitali hiyo ni miongoni mwa
hospitali chache zilizopo katika wilaya yake ambazo zinatibu magonjwa ambayo
yanaitajika kufanyiwa upasuaji.
Amesema Licha katika wilaya yake kuwa na hospitali
moja ya Amana ambayo pekee inatoa huduma
ya zaupasuaji ila amedai kuanzishwa kwa hospitali hiyo kutapunguza masongomano
wa wagonjw akatika Hospitali ya Amana jambo analodai litapunguza vifo vya mama
na motto vinavyotokea kwa kukosekana kwa hospitali za upasaji,
Sanjari na hayo Dk Sangu amewataka Watanzania
kuitunza hopstali hiyo ili iweze kuendelea kutoa matibabu kwa wingi.
Kwa upande waku Mkurugenzi wa Hospitali hiyo,Dk
Jerome Mkiramwani amewasema nia ya
Hopsitali hiyo ni kutoa matibabu kwa bei ya nchini kwa Watanzania huku
akiwataka wakazi wa Tabata kisukulu kujitokeza kwa wingi kupata matibabu kwenye
Hospitali hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni