CCM WAZIDI INYONGA DEMOKRASIA NCHINI,YAVURUGA TENA UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI LA DAR,SOMA HAPO KUJUA
Madiwani wa Chadema wakipambana na polisi katika ukumbi wa Karimjee baada ya uchaguzi wa Meya kuhairishwa
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wanashiriki kuvuruga utaratibu wa uchaguzi
wa Meya wa Jiji hilo, anaandika Happyness Lidiwno.
Sara Yohana, Kaimu Mkurugenzi
wa Jiji amehairisha tena uchaguzi wa Meya wa jiji hilo kwa mara ya nne sambamba
na matakwa ya CCM ambao tangu awali hawakuonesha nia ya kushiriki kwenye
uchaguzi huo.
Kabla
ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo, wanachama wa Ukawa walifika mapema na kuingia
kwenye Ukumbi wa Kareem Jee huku wanachama wa CCM wakijizoazoa kuingia ukumbini
hapo.
Theresia
Mbando ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo, alitoka nje na kuwataka
wajumbe hao wa CCM kuingia ukimbini ili mkutano huo kuanza.
Baada
ya CCM kuingia ndani, Mbando alifuata taratibu zote za kiitifaki katika
kufungua kikao hicho ikiwa ni pamoja na kugawa ratiba za mkutano huo.
Wajumbe
wakiwa tayari kwenda na ratiba ya mkutano huo, ndipo Sara (Kaimu Mkurugenzi)
alisimama ghafla na kutangaza kughairishwa kikao hicho.
Yohana
alidai kwenye maelezo yake kwamba, amepokea zuio kutoka Mahakama ya Kisutu
iliyomtaka kutoendesha uchaguzi huo.
“Tunaghairisha
uchaguzi huu kwa kuheshimu zuio la mahakama ambalo litadumu kwa miezi mitatu
hadi pale kesi ya msingi itakaposikilizwa ndipo tutaitisha tena uchaguzi,”
amesema Sara.
Mara
tu baada ya kauli yake, wajumbe wa CCM harakaharaka walisimama na kutoka nje
huku wakicheka wengine wakisema “hahahaaa, wajiju. Shoga kwaheri” huku
wakigonganisha mikono.
Wakati
Mwenyekiti na Kaimu Mkurugenzi wakijiandaa kutoka nje ya ukumbi, wananchi
pamoja na viongozi wa wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) waliwazuia
wakidai kupewa ufafanuzi zaidi wa zuio hilo.
“Hapa
huondoki hadi utuoneshe barua kutoka mahakamani, hakimu aliyetoa hilo zuio,
aliyefungua madai na sababu za kuzuia uchaguzi,” mjumbe mmoja wa Ukawa
alisikika akisema hivyo.
Si
mwenyekiti wala kaimu mkurugenzi aliyeweza kujibu maswali ya Ukawa, wakati huo
viongozi hao walikuwa wamezingirwa na ahama pia wajumbe wa Ukawa.
Kwa
mujibu wa viongozi wa Ukawa, zuio lililobandikwa lilikuwa ni la tarehe 5
Februari mwaka huu ambalo lilikuwa linazuia uchaguzi uliokuwa umepangwa
kufanyika tarehe 8 Februari mwaka huu.
“Kwanza
hata hivyo kama kweli uchaguzi haujafanyika kwa sababu ya zuio hilo kwanini
mkurugenzi aliitisha uchaguzi? Inamaana hakujua kama kuna zuio? Huu ni wizi na
ni njama baina ya CCM na Mkurugenzi” viongozi wa Ukawa walisikika wakilalamika.
Baada
ya vurugu kuzidi, polisi zaidi ya 15 waliobeba silaha wakaingia ukumbini na
kumtoa mwenyekiti kwa nguvu kwa kumpitisha mlango wa dharura na kupandishwa
gari lao kisha kutokomea.
Baada
ya vurugu kutulia, Ukawa walikaa kikao ambapo John Mnyika, Mbunge wa Kibamba
alitoa tamko ambalo liliazimiwa na vingozi wa Ukawa kwamba, wajumbe watawanyike
hadi tarehe 29 Februari ambapo wanatarajia kwenda mahakamani.
“Naombeni
tuondoke kwa amani, jumatatu tutawachukua madiwani watatu na mawakili wetu
kwenda mahakamani ili tuombe kuingia kwenye hiyo kesi. Tunaimani tutashinda
hata wafanye nini Jiji ni letu,” amesema Mnyika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni