WAZIRI WA MAGUFULI AFANYA UMAFIA KWENYE KIWANDA CHA NGOZI,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina |
NAIBU Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, amekifunga na kukipiga faini ya Sh. 25
milioni, kiwanda cha kusindika ngozi mjini Shinyanga cha Xing Xua kutokana na
ukiukwaji wa kanuni na sheria za Mazingira ya mwaka 2004. Anaandika Moses Mseti,
Shinyanga … (endelea).
Kiwanda hicho kinachomilikiwa
na raia wa kichina kimefungwa baada ya kubainika kinaendesha shughuli zake huku
kikiwa hakijakamilika, pamoja na mazingira yake yakiwa yana hatarisha afya za
wafanyakazi pamoja na wananchi wanaokizunguka.
Hata
hivyo kiwanda hicho kinachozalisha ng’ombe 2580 na mbuzi na kondoo 1,000 kwa
siku kimetelekezwa na wamiliki wa kiwanda hicho kutokana na upatikanaji wa
ngozi kuwa mdogo pamoja na kupanda kwa gharama ya ngozi kutoka kwa wachinjaji.
Akizungumza
jana mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya kukagua kiwanda hicho, Mpina
amesema kuwa kiwanda hicho kimekiuka sheria za uendeshaji pamoja na mazingira
ya kiwanda hicho kuwa machafu, kitendo ambacho kinahatarisha uhai wa wananchi
wanaoishi karibu na kiwanda hicho.
Mpina
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu, amesema kuwa mara nyingi
wawekezaji wamekuwa wakishindwa kufuata taratibu za uendeshaji wa shughuli zao,
na wakati serikali ikitaka kuwachukulia hatua hudai kwamba wananyanyaswa bila
kutambua kwamba wao ndiyo chanzo cha yote.
“Kwa
mamlaka niliyonayo na kwa mjibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004, natamka
kwamba kiwanda hiki kuanzia sasa nakifunga kwa muda kutokana na kukiuka Sheria
ya Mazingira mpaka pale kitakaporekebisha makosa yaliyopo kwenye kiwanda hiki
na wakishindwa kufanya hivyo hatua zitachukuliwa kwa wamiliki wa kiwanda.
“Pia
kuna sehemu ya shimo ambalo limerundikwa uchafu uliochanganyikana na vipande
vya ngozi, nyama na maji yenye sumu natoa siku saba eneo hilo liwe limefunikwa
maana ni hatari kwa afya ya binadamu, na matengeneze maeneo ya kitaalamu ya
kuhifadhia taka ngumu na siyo kuzitupa ovyo,” amesema Mpina.
Mratibu
wa (NEMC) Kanda ya Ziwa, Anna Masasi, amesema kiwanda hicho kiliomba kibali cha
kuchinja mifungo lakini cha kushangaza kinafanya kazi ya kusindika ngozi
kinyume na Cheti chao cha uwekezaji hapa nchini, huku akikitaka kibadili cheti
hicho kabla ya hatua kuchukuliwa.
Mwenyekiti
wa Mtaa Mpera ‘C’ Kata ya Ibadakuli mjini, Charles Sandu, amesema kuwa eneo la
kiwanda hicho limekuwa likitoa halufu mbaya na kwamba endapo hatua
zisipochukuliwa wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo wanaweza kuungua ugonjwa
mbalimbali huku wakimpongeza naibu huyo kwa hatua ya kukifunga kiwanda hicho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni