WAISLAM CHINI WALAANI MAUAJI YA MTETEZI WA DINI YA KIISLAM NCHINI SAUDI ARABIA,SHEIKH JALALA ATOA YA MOYONI,SOMA HAPO KUJUA
WAISLAM
nchini wamelaani vikali kitendo cha serikali ya Saudi Arabia cha kumuua
mwanadhuoni Ayotollah Sheikh Bagir Nimr ambaye alikuwa anawatetea
wanyonge na waislam nchini humu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akisoma tamko la kulaani kitendo hicho, Sheikh Hemed
Jalala ambaye ni Kiongozi wa chuo cha
kiislam cha (Hawaza) Imam Swadig, Sheikh
huyo pia ambaye ni mmoja wa viongozi
wakuu wa kiroho wa wailsamu dhehebu la shia Ithna asherriya Tanzania
Ambapo amesema waislam nchini wamepokea kwa
masikitiko makubwa kwa kitendo cha kinyama cha watu kumuua kwa kumchinja hadharani mtetezi huyo baada ya kuhukumiwa
kifo na serikali ya nchi hiyo.
Amesema
adhabu ya kifo aliyopewa mwanadhuoni huyo ni ya kionevu kwani haendani na
mafunzo ya dini ya kiislam.
“Yaani
huyo Sheikh Nimr amehukumiwa baada ya kutetea haki ya waislam ikiwemo
kupata haki ya kusari mara tano kwa siku
ambayo nchini Saudi Arabi hawapati nafasi hiyo,amekuwa anatetea haki ambayo
serikali yake ilikuwa haiwatendei haki wananchi wake,lakini leo serikali hii
ikaona njia sahihi ya kumyamazisha ni kumhukumu kifo “amesema Sheikh Jalala.
Waislam wa msikitiwa Kigogo Post Jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye sara ya kulaani unyama huo
Sheikh
Jalala akiongea kwa uchungu amesema inasikitisha kuona nchi kama Tanzania ambayo
inamuunganiko wa dini mbali mbali lakini bado waislam wanapata haki ya kuaabudu
mara tano kwa siku lakini nchi ya Saudi Arabia ambayo ni ardhi yake imetaliwa
na dini hiyo lakini waislam hawapati nafasi ya kuabudu mara tano kwa siku jambo
analosema linakwaza mtume Muhamed ambaye alitaka kila mtu apewa haki ya kuabudu.
“Makosa
yalitajwa na serikali ya Riyadhi juu ya Ayatollah Nimr na wenzake kwamwe
hayakustahili adhabu hiyo,kumuua kiongozi mwenye wafuasi kwa kosa la kudai haki
za wanyonge ni kuchochea vurugu”amesema
Sheikh Jalala.
Sheikh
Jalala amebainisha kuwa binadamu ni kiumbe aliyehuru kutokuwa na minyororo ya ukandamizaji na utumwa katika Nyanja
zote,yuko huru kutokuwa na utumwa wa kifikra, huku akihoji ni kuwa ni kivipi
karne hii ambayo uelewa juu ya masuala ya binadamu na maswala ya kielimu
yameshika kasi kwanini yatokea mambo kama haya.
Vilevile
Sheikh Jalala ameitaka Dunia kuingilia kati vitendo vya kinyama vinavyofanywa
na serikali ya Saudi Arabia kwa kunyima uhuru wa haki za kuishi pamoja na kutoa
maoni.
Mwanazuoni
Ayatollah Sheikh Bagir Nimr aliuwa tarehe 2/1/2016 baada ya kutolewa hukumu na
serikali ya Saudi Arabia baada ya
kuhukumu kwa kosa la kushiriki kudai hakiiii ya uhuru wa wananchi kuchagua
viongozi wao kwa kura badala ya kuongozwa kifalme,
Kosa jengine ni
kudai haki za binadamu ziheshimiwe kwa kuwa kuna matabaka ndani ya nchi ynanyima haki zao za
msingi,pamoja na kutolewa na kuachiwa huru wafungwa wakisaisa waliokamatwa kwa
kudai mabadailiko ya kiungozi katika serikali na haki ya kuchagua viongozi wao.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni