Zinazobamba

WIZARA YA MAGUFULI KUITIA HASARA SERIKALI BILIONI 124.8,PPRA WASEMA HASARA HIYO KUONGEZEKA,SOMA HAPO KUJUA


WIZARA ya Ujenzi imetajwa kuitia hasara serikali ya Tanzania jumla ya  Bilioni 124.8 kutokana na kuchelewesha kulipa deni la trilioni 5.3 kwa makandarasi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
            Hayo yamesema leo jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji mkuu wa Tume ya manunuzi ya Umma (PPRA) Dk  Shirima wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo  amesema tume hiyo imebaini hasara hiyo baada ya kufanya ukaguzi  kwenye Wizara hiyo ambayo inayongozwa na Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Dokta John Magufuli
           Na kukuta ucheleweshaji mkubwa wa kulipa deni  makandarasi husasani kwenye miradi ya ujenzi  wa barabara ya ujenzi  wa barabara nchini ya TANROADS  na miradi ya maji kwenye serikali za mtaa.
          Dk Shirima amebaisha kuwa jumla ya mikataba 301 ya TANROADS yenye thamani ya trillion 5.3 ilicheleweshwa malipo na hivyo kuwa na malimbikizo ya riba ya shilingi  Bilioni 124.8 hadi mwezi juni.2015.
         Hata hivyo Dk Shirima amesema riba hiyo itazidi kuongezeka hadi hapo malipo yatakapofanyika.
         Sanjari na hayo,PPRA imezitaja taasisi  9 ambazo zimekuwa na viashiria vya rushwa ya kutisha katika utendaji wake ikiwemo katika kufanya manunizi.
           Amezitaja taasisi hizo ni Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini,Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,Halmashauri ya wilaya ya Mpanda,Kampuni ya reli nchini TRL,Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo,Halmashauri ya wilaya ya kigoma,Halmashauri ya Wilaya Mbozi pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.
Katika Hatua nyingine PPRA imezifungia miaka miwili kampuni 6 pamoja na kufingia kampuni moja kwa kipndi cha Miaka 10 baada ya kubainika walifanya udanganyifu ikiwemo kufoji ili kupata tenda ya dhabuni.
          Kampuni sita hizo ni  M/s Intersysten Holding Company ,limited,M/s PEMA TECH Company Limite,M/S Nyakatire Investment Limetd.
Kampuni nyengine ni Kosemwa Propsects Company Limetd ,Ms Perntels Company Limited,MS Car  and general Trading Limited.

  


Hakuna maoni