TAARIFA KUHUSU JENERAL MWAMUNYANGE KUWEKEWA SUMU.UKWELI WAKE HUU HAPA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI kukiwa kuna taarifa zinazoenezwa kwa kasi
kwenye mitandao ya kijamii zikisema mkuu wa Majeshi ya ulinzi
nchini Jeneral Davis Mwamunyange kuwa amewekewa sumu na hali yake sahivi kuwa mbaya,,
Huku,taarifa
hiyo ikisema sababu ya kuwekewa sumu
huko, imetokana na masuala ya kisiasa,hatimaye Serikali imeibuka na kukanusha
taarifa hizo na kusema ni za uongo zenye nia ya kufakaranisha Taifa.
Akikanusha
Uvumi huo, leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Afisa Habari wa Serikali ambaye pia ni
mkurugenzi wa Idara ya Habari –Maelezo Assah Mwambene amesema Jeneral
Mwamunyange yupo salama na anaendelea na kazi zake,akidai kuwa taarifa hizo
zinalengo ya kuchonginisha watanzania na
jeshi na kuharibu picha ya Amani na utulivu uliopo nchini.
Pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Asssah Mwambene akizungumzana waandishi wa habari |
Mwambene
amewataka Watanzania kupuuza taarifa hizo huku akiwasihi kutoingiza siasa
kwenye masuala nyeti ya nchi ikiwemo jeshi,kwani jeshi ni taasisi isiyojihusiha
na siasa.
Wakati
huo huo pia Serikali imetolewa ufafanuzi juu ya taarifa zilizoandikwa kwenye Gazeti la Tanzania Daima ambazo zilikuwa zinaubeza uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais Jakaya
Kikwete kwa kuwateua wakuu wa wilaya wapya, wakidai uteuzi huo ulikuwa ni wakulipa fadhira kwa kwa wanachama wa Chama
cha Mapinduzi CCM.
Akifafanua
uteuzi huo,Mwambene amesema watu wanaobeza ni uteuzi huo watakuwa hawajui
sheria za nchi na kufahamu mamlaka ya Rais,
Amesema kwa mujibu wa sheria.kanuni za nchi na taratibu
Rais anamamlaka ya kufanya
uteuzi wakati wewote inapobidi kwa
malengo ya kuboresha utendaji wa kazi serikalini.
“Serikali imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na
gazeti la Tanzania daima kuhusiana na uteuzi
wa Rais,taarifa hizi ni za kichochezi na zinalenga kumchonganisha Rais
na wananchi wake”amesema Mwambene.
Aidha,Mwambene
amevitaka vyombo vya habari nchi kufanya utafiti na kusoma kabla ya kuandika habari
,na pia akavihasa kuandika habari zenye
lengo la kujenga umoja na mshikamo badala ya kuandika habari zenye lengo
kuwagawa Watanzania
Hakuna maoni
Chapisha Maoni