WANANCH WAMSAIDIA KIKWETE KUVUNJA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI,WAENDELEA KUWANG'OA MAWAZIRI WAKE,SOMA HAPO KUJUA
NI kama wananchi wameamua kumsaidia Rais Jakaya
Kikwete kuvunja baraza la mawaziri,ndivyo naweza kusema baada ya hivi sana
mawaziri wake kuendelea kuanguka kwenye majimbo mbali mbali ya ubunge,
Ambapo tena Waziri wa sayansi na mawasiliano,Profesa
Mbarawa kuangushwa rasmi kwenye nasafi ya yake ya Ubunge kwenye nafasi ya
kusini pemba baada ya mgombea wa Cuf kumbwaga kwenye nafasi hiyo
Mbarawa anaungana na wenzake ambao ni anaungana na wabunge wengine maarufu wa Bunge
la Kumi walioshindwa kutetea majimbo yao, wakiwamo wa kambi ya upinzani ambao
wameangushwa na wagombea wa CCM.
Pia wamo mawaziri wa zamani wawili, Cyril Chami na Omary Nundu
walioanguka kwenye uchaguzi, kwa mujibu wa matokeo ambayo yanaendelea
kutangazwa.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema jana kuwa itakamilisha
kazi ya kutangaza matokeo yote keshokutwa.
Mawaziri walioanguka kwenye uchaguzi huo ni Steven Wasira,Christopher Chiza, Aggrey Mwanri, Dk Steven Kebwe na Anne Kilango.
Katika matokeo yaliyotangazwa jana, Wasira, kada maarufu na
mwanasiasa mkongwe aliyekuwa akitetea Jimbo la Bunda, alijikuta akiangushwa na
mwanasiasa kijana, Ester Bulaya, ambaye alihamia Chadema baada ya Bunge la Kumi
kumaliza muda wake.
Wasira, ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo na Chakula, alianza
mchakato wa uchaguzi mwaka huu kwa kuomba ridhaa ya CCM agombea urais, lakini
hakupitishwa. Bulaya, ambaye alikuwa mbunge wa viti maalum (CCM), alipata kura
28, 508 na kumuacha mbali waziri huyo mkongwe aliyepata kura 19, 126.
Mwingine aliyeanguka ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-
Uwezeshaji na Uwekezaji, Christopher Chiza ambaye ameangushwa na Bilago Samson
wa Chadema katika Jimbo la Buyungu. Waziri huyo alizidiwa kwa kura 104 baada ya
Samson kupata kura 23,041 dhidi ya 22,934 za Chiza.
Lakini hali haikuwa hivyo kwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey
Mwanri kwenye Jimbo la Siha. Waziri huyo alizidiwa kwa zaidi ya kura 4,100 na
mpinzani wake kutoka Chadema, Dk Godwin Mollel aliyepata kura 22,746.
Katika Jimbo la Serengeti, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk Stephen Kebwe pia alijikuta akipoteza nafasi ya kurudi bungeni kwa
kura alipoangushwa na Marwa Ryoba wa Chadema. Dk Kebwe alipata kura 39,232,
akiwa amezidiwa na mpinzani wake kwa zaidi ya kura 820.
Anne Kilango, ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu mwaka
2013 baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyosababishwa na kashfa ya
Operesheni Tokomeza, ameangushwa na mgombea wa Chadema, Naghenjwa Kaboyoko wa
Chadema kwa tofauti ya kura 3,297.
Kilango alipata kura 15,539 wakati mgombea huyo wa Chadema
alipata kura 18,836. Pia wabunge maarufu kama Vincent Nyerere (Musoma Mjini),
James Lembeli (Kahama Mjini) na Kyisieri Chambiri (Babati Mjini) wameangushwa.
Nyerere, aliyekuwa akitetea kiti cha Musoma Mjini kwa tiketi ya
Chadema, aliachwa mbali na mgombea wa CCM, Vedastus Mathayo aliyepata kura 32,
836 dhidi ya 25,549.43 za Nyerere.
Lembeli, ambaye alihamia Chadema muda mfupi baada ya Bunge la
Kumi kumaliza muda wake, aliachwa mbali na mfanyabiashara maarufu, Jumanne
Kishimba aliyepata kura 47,553 dhidi ya kura 30,122 za Lembeli.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni