KAFULILA AZIDI FANYIWA HUJUMU,MWENYEWE ASEMA AMESHINDA ISIPOKUWA,SOMA HAPO KUJUA
DAVID KAFULILA
TUME INATAKA KUNIHUJUMU KIGOMA KUSINI.
Kwanza Mkuu wa Mkoa Kigoma Kanali Issa Machibya na Mkuu wa
Wilaya Mrisho Gambo walifanya kampeni kubwa na vitisho kwa wananchi wakitumia
polisi.
Pamoja na hujuma zote hizo bado majumuisho kwa fomu za mawakala
nimeongoza kwa kura 2435.
Kwa kujua hilo jana mgombea wa ccm Hasna Mwilima amekuja kukataa
matokeo ya baadhi ya kata na kutaka zihesabiwe upya. Nikakataa kwa nguvu zote
na nikamuonya msimamizi ache kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa.
Msimamizi akamua kusitisha zoezi la majumuisho na kwamba
anamwandikia barua Mkurugenzi wa uchaguzi taifa kwa mwongozo.
Msingi wa kukataa kuhesabu upya matokeo ni ukweli kwamba fomu za
mawakala tunazo na hazina kasoro.ccm hawana fomu za mawakala wao.
Lakini sababu ya pili sina imani na masanduku kwamba
hayajachakachuliwa kwani tangu baada ya kupiga kura yalikuwa chini ya polisi na
tume wenyewe bila wakala. Na hili linakuwa na uzito kwasababu ya taarifa za
magari ya kura feki yaloingizwa chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa na wilaya
Msimamo wangu ni kwamba sipo tayar kufungua masanduku na
kuhesabu upya ni bora msimamizi akili ameshindwa kusimamia zoezi na uchaguzi
ufutwe kuliko kuhesabu masanduku ambayo sina hakika nayo.
Naomba umma ujue haya kwa ufafanuzi wa kinachoendelea kwani
mpaka sasa wamejaza polisi eneo hili kiasi cha kutisha.
Tulianza na Mungu na Hakika tunamaliza na Mungu.
David Kafulila
Hakuna maoni
Chapisha Maoni