HATIMAYE GWIJI LA HABARI NCHINI LAINGIA BUNGENI RASMI,NI SAED KUBENEA,SOMA HAPO KUJUA
HATIMAYE
mwandishi wa habari hodari nchini,Saed Kubenea amefanikiwa rasmi kuingia
bungeni baada ya kushinda ubunge kupitia jimbo la ubunge na kumbwaga kwa
kishindo mpinzani wake kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dk Didas Masaburi.
Kubenea ambaye alikuwa nagombania kupitia chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema, amemshinda Meya huyo wa zamani mkoani Dar es
Salaam kwa ushindi wa kura 87,777 na huku masaburi akiambulia kura 59,640.
Kuibuka huku ushindi
kwa mwandishi mwandamizi nchini saed Kubenea kunakuwa ni kama pigo kwa Rais
Jakaya Kikwete na familia yake,ambapo kubenea mara kwa mara kwa kutumia magazeti
yake bora ambayo ni Mwanahalisi pamoja na Mawio kuripoti madudu yalikuwa
yanafanywa na watendaji wake.
Kwenda huku kwa
kubenea Bungeni kunazidi mtikisa Rais Kikwete kutokana na Kubenea kutamba pindi
akifanikiwa kuingia bungeni atafichua madudu anayodai yalikuwa ynafanywa na
watendaji kwenye utawala warais Kikwete.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni