MAMA ANA MGHWIRA AMKABIDHI ILANI YA CHAMA CHA CHAKE MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
ALIYEKUWA
Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Anna Mghwira amekubali kushindwa
katika kinyang’amyiro cha Uchaguzi Mkiuu na amemtaka Rais mteule, Dk. John
Magufufuli kushughuliki uchumi wa nchi kwa maslahi kwa wananchi, Anaandika Faki Sosi …
(endelea).
Amezungumza hayo alipokuwa katika sherehe za
kukabidhi cheti cha ushindi kwa Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
John Magufuli kwenye Ukumbi wa Diamond Jublee Jijini Dar es Salaam.
Nghwirwa amemtaka rais huyo mpya kuleta mabadiliko ya uchumi wa
nchi kupitia ilani ya chama cha ACT-Wazalendo kwa kuzingatia uzalendo wa
kutumia vizuri rasilimali za taifa.
Akimakabidhi ilani ya chama hicho, Mghwira amesema kuwa ilani
hiyo ilizingatia usawa wa kijinsia kuwatengeneza benki za wakulima, kuweka
miiko ya uongozi kwa kuzingatia uadilifu.
Wagombea wengine waliohudhuria ni Chief Lutalosa Yemba wa ADC,
Fahmi Dovutwa wa UPDP, Macmillan Lyimo wa TLP, Janken Kasambala wa RNA.
Wasiohudhuria ni Hashimu Rungwe wa Chaumma na Edward Lowassa wa Chadema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni