DUUUUU LOWASSA NI HATARI,ARUSHA YASIMAMA,KINGUNGE AMCHALAZA KIKWETE NA CCM YAKE,SOMA HAPO KUJUA
Unga Ltd leo Alhamisi 8/10/2015
KADA Mkongwe wa Chama cha Mapinduzi CCM,Kingunge Ngombale –Mwiru ambaye amekiaga chama hicho ,ameendelea kukitolewa lawama cha hicho kusema CCM pumzi yake imefikia mwisho na hakitakiwi kupewa tena dhamana ya kuongoza nchi.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizungumza
wakati wa Kampeni za kumnadi Mgombea
Urais kupia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa mkono na
Vyama vya Ukawa,Edward lowassa zilizofanyika leo Arusha Mjini na kushuhudiwa na
umati mkubwa wa watu ambao uliosababisha shughuli nyingi kusimama.
Ambapo Kingunge amedai chama chake hicho kilichomlea
kimechoka na hakina nia ya kweli ya kumkomboa mtanzania anayeishi kwenye lindi kubwa la
umasikini.
Amesema CCM anayoijua yeye tangu ilipokuwa
TANU ilikuwa yenye misingi na kuweka mipango ya kumletea maendeleo moja kwa
moja Mtanznaia, lakini amedai CCM hile sio hii ya sasa kwani hii ya sahivi imetekwa na
watu wachache wenye kujali maslahi binafsi na sio kumleta maendeleo mtanzania.
Kingunge
huku akishangiliwa kwa nguvu,amemshukia pia Rais Jakaya Kikwete kwa kusema
utawala wake umeua uchumi wanchi,
“Leo uchumi wa nchi umeporomoka,wakati Mkapa
anamwachia nchi Kikwete uchumi ulikuwa kwenye hali nzuri,lakini baada ya
kuingia yeye uchumi wan chi umedorola huku umasikini unazidi kuwa mkubwa kwa
watanzania’
SUMAYE
ANENA.
Kwa upande wake Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya
tatu,Fredrick Sumaye amewataka watanzania kutomchagua Mgombea wa Urais kupitia
CCM John Magufuli kwani mgombea huyo anamaamuzi ya kukurupuka na ambaye tena asiyekubali kushaulika jambo ambapo amewasihii
Watanzania wakimchagua kuwa watakuja juta.
Sumaye ambaye ni waziri mkuu peke aliyeongoza kipindi kilefu amesema hata
wizara alizopewa Magufuli
kuongoza ameonyesha utendaji wa kibabe usiofuata utu na uzalendo kwa
watanzania.
LOWASSA
ANADI SERA.
Kwa upande wake Mgombea wa Urais kupiatia mwavuli wa
Ukawa Edward Lowassa amesema endapo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha
anapambana katika kuondoa umasikini kwa watanzania.
“Ninagombania nafasi ya Urais kutokana na kuchoka
kusikia habari ya Umasikini,nimedhamilia kupambana na umasikini,nimechoka
kusikia watu wanakula mlo mmoja,nataka nikiingia tuwe tunajadili milo
mitatu,ambaye ana ngombe mmoja awe na Ngombe wa wili”amesema lowassa.
Lowassa pia ameendelea kushikilia ilani yake ya
elimu bure kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu huku akiwapinga wanaibeza ahadi
yake hiyo kwa kusema nchi hii inapesa nyingi zinazopotea kwenye Mgari ya
kifahali.
KUHUSU
TANESCO.
Lowassa amesema endapo akifanikiwa kuingia
madarakani atahakikisha analifufua shirika la Umeme nchini TANESCO ndio
litakuwa jambo lake la kwanza na kulifanya shirika hilo liondokane na mgao wa
umeme.
LEMA
AFUNGUKA.
Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjinia
kupitia Chadema Goodbress Lema ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC
kupeleka haraka karatasi za kupigia kura kwenye mkoa wa arusha ili wananchi
wawajue wagombea wao.
Amesema kwa sasa wananchi wa jimbo hilo la Arusha
wamezamilia kwa kauli moja kumchagua Lowassa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni