Zinazobamba

FLAVIANA MATATA :AUKWAA UBALOZI WA UTALII NCHINI MAREKANI


Katibu mkuu Wizara ya mali asili na utalii Abdelhelm Meru (kushoto) akimkabidhi Flaviana Matata (Kulia) barua ya uteuzi. Jijini Dar es salaam
DAR ES SALAAM
WIZARA ya mali asili na utalii nchini ime mteua rasmi Mwana mitindo Flaviana Matata kuwa balozi wa kuutangaza utalii katika Jjiji la Newyork Nchini Marekani
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katibu mkuu wa wizara hiyo Adelhelm James Meru amesema hatua ya kumteua Flaviana ni utekelezaji wa tangazo jipya la utalii lililo  zinduliwa na Rais Kikwete tarehe 4 septemba mwaka huu
Akizitaja sababu za uteuzi wa mwana mitindo huyo kuutangaza utalii nchini Marekani amesema wiza hiyo imepitia takwimu kwa kina na kubaini watalii wengi wanatokea nchini Marekani na kwamba wameona ni vema kumtua mwana mitindo huyo wa kitanzania  kwa kuwa ana sifa ya uzawa na hivyo kupitia yeye wana amini ata vitangaza vivutio vilivyopo nchini katika shughuli zake
Kwa upande wake Flaviana Matata ameishukuru wizara kwa uteuzi huo, amabpo ame wahakikishia watanzania kuwa ata itumia fursa hiyo kikamilifu ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha pato la taifa linakua mara dufu
Sekta ya utalii nchini inachangia fedha za kimarekani takribani billioni 2 sawa na asilimia 25, ambapo kwa sasa sekta hiyo imeajiri asilimia 10.2 ya watanzania

Hakuna maoni