Zinazobamba

WATUMIAJI WA "MIKOROGO" HATARINI,TFDA YASEMA HALI NI MBAYA,SOMA HAPO KUJUA

pichani ni Mkurugenzi wa (TFDA) Hiiti Sillopicha na Maktaba

MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imewahatazalisha watumiaji ya “mikorogo”  nchini kwa kusema wako hatarini kupata kansa ya ngozi.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
            Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa (TFDA) Bwana Hiiti Sillo wakati akifungua mkutano na wadau mbali mbali wa uigizaji vipodozi nchini, ambapo amesema Mamlaka yake kwa sasa imebaini kuwepo kwa watu wanaotumia  “mikirogo”  ya asili ambayo inamatatizo.
         Sillo ameyataja matatizo hayo ni pamoja na  kuwepo na kemikali kali,zinazopatikana  katika uchanganyaji wa mikorogo hiyo ambazo zinapelekea magonjwa mbali ya kansa ya ngozi.
        Amesema kwa sasa TFDA kwa kushirikiana na vikosi kazi mbali mbali  vimepanga kuhakikisha wapiga vita matumizi ya mikorogo kwa Watanzania.
       Aidha,Mamlaka hiyo imesema katika mwaka wa fedha uliomalizika wamafanikiwa kukamata Dawa feki pamoja na vipodozi vilivyoingia nchini, zaidi ya Tani 16 zenye thamani ya milioni 49 na kuziteketeza zote.

Hakuna maoni