|
Wakati mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF akitarajiwa kuongea na wanahabari muda mchache ujao kuhusu ushiriki wa chama chake ndani ya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wanachama mamia wamevamia ofisi za chama hicho zilizopo hapa hapa BUGURUNI wakiimba nyimbo mbalimbali zakuonyesha kuwa wanaimani na mwenyekiti huyo ndani ya chama hicho.
Kumekuwa na sintoifahamu mbalimbali juu ya Chama hicho kujiengua au kubakia ndani ya muungano huo huku magazeti kadhaa jana yakiriport kuwa mwenyekiti huyo amejiuzulu nafasi yake ya uenyekiti ndani ya chama hicho kutokana na shinikizo la wanachama wake.
Hakuna habari zozote zilizodhibitisha habari hizo ila macho na maskio ya watanzania tuelekeze hapa atakapozungumza na wanahabari kujua mbivu na mbichi.Picha hizi zinaonyesha hali ilivyo sasa ndani ya makao makuu ya chama hicho |
ENDELEA KUFUATLIA MTANDAO HUU UTAPATA TAARIFA KAMILI
MWANDISHI WAKE KAROLI VINSENT ATAKUPA TAARIFA KAMILI.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni