TNGP YAZIDI WABANA WANASIASA,YATOA TAMKO ZITO,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa TNGP Lilian Liundi akisema jambo wakati wa Kongamano la maji 2015 |
WANAHARAKATI
wa Mtandao wa kijinsia nchini (TNGP) wametoa kauli moja kuwa hawata kiunga
mkono chama chochote cha kisiasa ambacho hakitazungumzia suala la maji katika
kampeni zake zinazotarajia kuanza mwishoni mwa wiki hii.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo
Msimamo huo umetangazwa leo Jijini
Dar es salaam na Mkurugenzi TNGP Lilian Liundi wakati wa Kongamano
linalojulikana kwa jina Maji mwaka 2015 ambapo amesema kwa kipindi kirefu
wanasiasa wamekuwa wakiwahadaa watanzania katika kipindi kama hiki cha uchaguzi kwa kutumia ahadi ya maji kama njia ya kupata kura lakini pindi wanapochaguliwa
anadai wanakuwa wagumu kutekeleza ahadi hiyo.
Waharakati mbali mbali wanahusika na masuala ya Maji wakiwa makini kumsikiliza Bi Liundi |
Amesema wanaharakati wamekuwa
wakipigia kelele suala la maji lakini bado wanasiasa wamekuwa wakiwapuuza sasa wamedai
wanakuja na mipango ya kuchukua hatua ikiwemo kuwakataa wanasiasa watakoshindwa
kutekeleza ahadi ya maji.
Amebainisha kuwa kwa sasa njia
watakayotumia ni kuwapima wanasiasa hao na kuwafatilia pindi watakapochaguliwa
ili kujua kama ahadi hiyo ya maji itatekelezwa.
Kwa Upande wake Mwanaharaki wa
haki za Binadamu kutoka ndani ya Mtandao wa TNGP Mama Akilimali naye amewataka
wanawake kutopweteka katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu kuungana kwa pamoja kuhakikisha ahadi ya maji inatekelezwa
kivitendo
wanaharakiti wengine wakiwa makini kufuatilia kongamano hilo |
Mwanahaharaki huyo amesema nguvu yoyote katika nchi yoyote inatokana na mwananchi mwenyewe na sio kwa viongozi,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni