Zinazobamba

TNGP YAWACHARUKIA WANASIASA,YASEMA MDA WA KUVUMILINA UMEPITWA NA WAKATI,SOMA HAPA KUJUA


Pichani ni Mkurugenzi wa TGP Lilian Liundipicha na Maktaba
MTANDAO wa Kijinsia nchini (TNGP) umesema hautokubali kuwaacha wanasiasa wakitoa ahadi za uongo kwenye suala la maji katika kampeni za uchaguzi zinatotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu na kusema wataifuatilia ahadi hiyo mpaka mwisho.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
           Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa (TNGP) Bi Lilian Liundi wakati wa kufungua semina iliyowashirikisha wadau mbali mbali nchini wa masuala ya Maji yenye lengo la kuwajengea uwezo katika uchaguzi  ambapo Bi  Liundi amesema kwa sasa nchini mda wa kuvumiliana umepita kwani katika chaguzi nyingi zinazopita -,
              Wanasiasa wamekuwa wakitumia ahadi ya kuwapatia wananchi huduma ya maji kama nyenzo ya kupata madaraka lakini pindi wakipata madaraka hayo wanaisahua ahadi hiyo.
              Amesema licha ya kutotekelezwa kwa ahadi hiyo mzigo mkubwa unamwangukia mwanamke ambaye ndio mlezi wa familia ukizingatia maji ndio kitu cha msingi katika usalama wake na kudai kwa kipindi  hiki wamejipanga kuhakikisha ahadi hiyo wanaifuatilia mapaka mwisho.
                  Pamoja na hayo amebainisha kuwa kwa sasa Wanaharakati hao baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo watagawanyika kila jimbo nchini na kufuatilia ahadi hizo na kuhakikisha zinatekelezwa na kwa vitendo.

                 Aidha,Bi Liundi amewakata wanawake nchini kutubweteka katika kipindi hiki cha Kampeni kwa kuwataka kujitokeza kwa wingi kwenye Kampeni hizo na kuwasikiliza wagombea wangazi zote ikiwemo Urais,Ubunge pamoja na Udiwani na kuhakikisha wanasikiliza kwa makini sera zao na kumchagua kiongozi atakayeweka maslai Wanawake mbele.

Hakuna maoni