TBC ONE YAANZA KUJIKANYAGA NA LOWASSA,YAUNGANA NA GAZETI LA UHURU KUMSAPOTI MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
KITUO cha Telivisheni kinachomilikiwa na kodi
za Watanzania cha TBC one kimeanza kumsapoti
mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM John Magufuli na kumtupilia
mbali mgombea wa vyama vya Upinzani
Edward Lowassa. ndivyo naweza kusema, Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yamebainika katika vipindi
mbali mbali vya TBC one ikiwemo taarifa zake za Habari,ambapo taarifa hizo za
habari zimekuwa zitoa nafasi kwa mgombea mmoja wa CCM na kuacha upande mwengine wa wagombea wa Urais,huku ikitazamiwa chombo hicho cha umma kutakiwa kuto kuwa na upande wowote na ikizingatia
chombo hicho kinaendesha kwa kila kitu na kodi za watanzanaia ambao wengine ni
wanachama wa Upinzani.
Katika jambo ambalo linazidi tia
shaka na kuendana na matakwa ya mtazamo wetu uliendelea kuenekana katika
kipindi cha kuchambua magazeti kilichorushwa leo asebuhi ambapo-
Mtangazaji wa kipindi hicho, hakusoma magazeti
ukrasa wa kwanza na kusoma ukrasa za
ndani kwa kuwa ukrasa wa mbele wa magazeti hayo yalikuwa na habari iklionyesha
umati wa watu katika mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia Chadema Edward Lowassa
uliofanyika mkoani mbeya .
Mtoa taarifa wa mtandao huu aliyekuwa
ndani ya TBC one ameambia mtandao huu ni kwamba hilo limekuwa ni shinikizo la
watu wachache.
“Yaani hata
sisi tunashangaaa sana wakati wa Magufuli anachukua fomu ya Urais tulisoma
magazeti ukrasa wa kwanza na huo utamaduni wetu,tunashangaa sasa tunabadirika
na kuzikimbia kuzisoma habari za upinzani mpaka tunashangaa,huko nje jamii itatuchukuliaje”kimesema
chanzo chetu hicho.
Licha ya kuwatupa wapinzani kiasi hicho
lakini, Mara kwa mara kituo hicho
kimekuliwa kililiwa na Viongozi wa Upinzania Bungeni akiwemo Waziri kivuli wa
Wizara ya habari na utamaduni na michezo Joseph Mbilinyi (Sugu) ambaye amekuwa
akiitaka serikali kuiongezea bajeti ili ifanye kazi kwa kisasa lakini kituo
hicho kimeshindwa hata kukumbuka hali hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni